Hasira Siku Zote Huzaa Hasara

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi ...

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Siku moja baba ammoja aliyeitwa Nick kabla hajatoka ofisini kwake, alinyanyua simu na kumpigia mkewe mpenzi aliyeitwa Roine na kumwambia, "Mke wangu mpenzi,leo jioni tafadhali usihangaike kupika chakula cha usiku kwa sababu nimejiandaa kuleta chakula kitamu sana kutoka kwa Mke wa Pili."

Baadaye jioni Mume alirudi nyumbani na chakula kama alivyomuahidi mke wake. Alipokaribia mlangoni alianza kuugonga. Mkewe alifungua mlango vizuri na kumpokea mme wake kwa kumshambulia kwa kumpiga bila kumuuliza swali lolote hadi akazirai na kupelekwa hospitalini ambako alilazwa akiwa hoi katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU-Intensive Care Unit).

Baada ya kuchunguza kwa kina iligundulika kuwa kumbe "Mke wa Pili" (Second Wife) ni jina la mgahawa ambao mke wa Nick hakuujua. Mgahawa huo uliitwa "The Second Wife Restaurant."

Hii stori inatupa m kuwa tusikurupukerupuke hovyo na hasira zetu kufanya jambo kabla ya kufikiria au kufanya utafiti wa kutosha kwani mwisho wake huwa usiyo mwema bali ni hasara tupu.

Vilevile, hadithi hii inatukumbusha kuwa, hasira hasara. Tufikirie japo kidogo kabla ya kutenda jambo lolote wakati tukiwa tumejawa na hasira.

Aidha, "majuto ni mjukuu," Roine alisikika akisema kwa kujuta na kusikitika.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Usimuamini Mtu Yeyote Asilimia Mia Moja

Next
Next

Majina Yana Maana Hasi Ama Chanya?