Usimuamini Mtu Yeyote Asilimia Mia Moja

Simulizi ...
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Dada mmoja alikuwa ameolewa na kaka mmoja hapa mjini. Maisha yao yalikuwa ni mazuri sana. Kwa kweli walipendana mno kiasi kwamba mume alikuwa hata anabeba mtoto wap mgongoni, jambo ambalo watu wengi walikuwa wanashangaa.
Mke alifikia mahali na kuona kuwa wenzake ambao walikuwa hawatendewi hayo na waume zao walikuwa hawajui namna ya kuishi na waume zao. Maisha yaliendelea vizuri. Aliwashangaa sana na kujiuliza kuwa wanawezaje kuishi na wanaume wasiokuwa na upendo.
Siku isiyokuwa na jina mke huyo alishangaa alipoletewa mtoto wa kiume ambaye alikuwa ni copyright ya mumewe. Yule dada alipagawa na kuchanganyikiwa vibaya. Tatizo la afya ya akili likampata. Kwa bahati mbaya hakuweza kupata unasihi mapema. Hatimaye umauti ulimfika.
Hadithi hii ni ya kweli, imetokea mwezi uliopita hapa jijini Dar es Salaam. Jambo la muhimu la kujifunza hapa ni kwamba rafiki wa leo ni adui wa kesho, tuwe makini sana. Yakupasa kuuamini moyo wako na sio moyo wa mwenzio. Katika maisha tusijisahau kwani yanaweza kutukuta sote. Maisha ni kitendawili.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania