Uaminifu Katika Ndoa

Simulizi ...
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Palitokea binti mmoja alichumbiwa na kijana mwenzie. Kwa bahati mbaya, uchumba wao haukudumu, wakaachana. Haikuchukua muda binti akapata mchumba mwingine aliyetokea mbali na mjini na hatimaye aliolewa naye. Mungu si Athuman, kijana mchumba wa kwanza wa binti naye alipata mchumba, akaoa. Mambo yakawa mazuri pande zote mbili.
Binti alipoolewa aliishi hapo hapo mjini ambako wazazi wake walikuwa wakiishi. Familia aliyoolewa huyu binti huyu ilikuwa ni familia nzuri na yenye uwezo. Wakwe zake walikuwa wanampenda sana.
Maisha ya binti yalikuwa ni mazuri mno. Alikuwa anapata fursa ya kuwatembelea wazazi wake mara kwa mara. Wakati alipokuwa akija kuwatembelea wazazi wake alikuwa anakutana kwa siri na yule kaka ambaye alikuwa mchumba wake wa mwanzo ambaye waliachana. Kwa kifupi, alikuwa anaendelea naye kimahusiano. Kutokana na mahusiano hayo ya siri na yule kijana,safari za kwenda kwa wazazi wake ziliongezeka kwani alikuwa anakwenda karibu kila siku. Akiomba ruhusa kwa mumewe ya siku tatu kwenda kuwaona wazazi wake basi atakaa siku mbili tu na siku ya tatu atakwenda kulala kwa yule mchumba wa zamani.
Siku moja aliomba ruhusa ya kwenda kwa wazazi wake lakini hakufika huko. Aliamua kupitia kwa huyo bwana kwanza kabla ya kwenda kwa wazazi. Kama waswahili wasemavyo: “siku za mwizi ni arobaini”. Ya arobaini ilimfika binti huyu. Kwa bahati mbaya binti alikutwa na umauti kwa huyo kijana. Kwa sababu kijana hakuwa akiishi mbali na kwa wazazi wa binti, majirani walienda kuwataarifu wazazi wake. Kwa mshituko mkubwa, wazazi walilazimika kufika kwenye eneo la tukio. Ilikuwa ni aibu tupu pale mtaani, kila mtu alipigwa na butwaa. Badala ya kuwa msiba wa heshima uligeuka kuwa msiba wa minong’ono, kila mtu akiwa na hadithi yake ya kusimulia, kila mtu akiongeza chumvi anayotaka ili mradi simulizi ipendeze kwenye masikio ya watu. Ilikuwa ni hali ya kutatanisha umma wa pale mjini.
Tunajifunza mengi kwenye mkasa huu.
- Hakuna siri duniani, hata ufanye mambo yako chini ya bahari yatakuja kujulikana tu siku moja. Yule binti alijiona kuwa mjanja na mwenye akili lakini yaliyompata baadaye ni ishara mbaya ya udanganyifu. Alifia kwa bwana ambaye si mume wake. Kifo kilimuumbua, kikatoa siri. Kifo chake pia kiliwatia aibu wazazi wake maskini ambao walikuwa hawajui mambo yaliyokuwa yakiendelea na binti yao.
- Tunajifunza umuhimu wa wazazi kuwafundisha watoto wao somo la uaminifu tokea watoto wangali wadogo. Misingi ya iaminifu inatakiwa kupandwa mapema kabisa kwa watoto wetu. Uaminifu kwa kila kitu, uaminifu wa kila mahali. Yawapasa watoto waogope kudanganya tokea wakiwa wadogo hadi ukubwani, hii ni pamoja na kuwa wakweli kwa wenzi wao.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania