Tusiwadharau Watoto, Wanaweza Kuwa Walimu Wetu Pia

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi ...

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Palikuwa na bibi mmoja ambaye alikuwa anaishi na mkwe wake kwenye nyumba moja. Siku moja bibi huyo alipokuwa anakula wali kwenye sahani ya udongo ilimponyoka, ikadondoka na kuvunjika. Mkwe wake alikuja haraka huku akiwa amefura kwa hasira. Akiwa amekasirika kama mbogo aliyejeruhiwa, alimuuliza mkwe wake, “Mama ndio umefanya nini tena? Mpaka sasa umekwishavunja sahani zangu nyingi mno, hata siwezi kuhesabu. Kama huwezi kunyanyua sahani, ni vema ukalia chakula mezani. Hii tabia ya kuangusha angusha na kuvunja vunja vyombo vyangu itaendelea mpaka lini? Kwa kweli, nimechoka, nimechoka sana.”

Mjukuu wake aliyekuwa anafanya mazoezi ya shule alipomsikia mama yake akimfokea hivyo bibi yake aliumia sana. Kwa haraka alifungua kikasha chake ambacho huwa anajiwekea vijisenti kwa ajili ya akiba yake, alichomoka upesi upesi kuelekea nje. Kwa mshangao mama yake alimnasa akiwa kwenye harakati za kutoka nje haraka, alimuuliza, “mwanangu unakwenda wapi”? Kwa upole akamjibu mama yake, “Nakwenda hapo mara moja dukani kununua kitu”. Aliendelea kusema kwa woga, “Mama, nafikiri labda wali uliluwa wa moto sana ndiyo maana bibi kadondosha sahani.”

Mama kwa ukali akamjibu mtoto wake, “Kwani unajua nini wewe?. Unafikiri fedha za kuhudumia familia zinapatikana hovyo hovyo tu ili wengine wawe wanavunja vunja tu sahani zangu?”

Maneno hayo yalizidi kuupasua moyo wa mtoto. Aliondoka haraka haraka, hata mama yake alipotaka kumzuia tena alikuwa amekwishatoweka.
Alipofika dukani, alinunua sahani mbili za aluminium ambazo huwa hazivunjiki. Aliporudi nyumbani alimkuta bibi yake akiokota ule wali pamoja na vipande vya sahani. Mjukuu alichukua kitambaa, akamfuta bibi yake mikono, kisha akachukua sahani moja kati ya zile mbili na kumpa bibi yake. Bibi alifurahi sana na akamshukuru mjukuu wake huku machozi yakimtoka.

Mama akamwuuliza mtoto,"Wewe ulienda wapi?” Mtoto akamjibu kwa heshima, “Mama yangu nilikwenda dukani kununua sahani za aluminium zisizopasuka ili usiendelee kukasirika kila siku. Kukasirika kila siku kunaathiri afya ya akili. Sahani moja nimempa bibi na nyingine ninakupa wewe.” Mama alikasirika sana, akamwambia mtoto, "Hivi wewe mtoto una kichaa nini? Mimi siwezi kuvunja sahani hata siku moja, kwa nini uninunulie na mimi sahani isiyovunjika”?

Mtoto akamjibu mama yake kwa heshima, tena bila kuogopa, "Nimekununulia kwa sababu na wewe utakapozeeka unaweza kupasua sahani kama bibi. Kwa hiyo na wewe kama utakuja kuishi kwetu sisi, yaani kwa mimi na mke wangu utatumia sahani hii ya aluminiam isiyovunjika. Mke wangu hatakasirika wala hatakuchukia kwani utakuwa unatumia sahani hii ya aluminium. Hivyo mke wangu hatakugombeza kwa kumvunjia vyombo vyake. Tafadhali mama, pokea bakuli hii na uitunze vema ili ije ikufae baadaye.” Mama alitahayari, aliinamisha kichwa chake huku machozi yakimdondoka.

Kutokana na mazungumzo haya tunakumbushwa kuwaheshimu na kuwathamini wazee. Hao unaowaona ni wazee leo walikuwa vijana kama wewe. Na wewe unayejiona ni kijana leo upo muda, upende usipende, utazeeka.

Yatupasa kukumbuka kuwa "Wakati ni ukuta,” kila mtu hana budi kuzeeka siku moja. Wakati tu ndiyo unaotofautiana.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Wazazi Wapendeni Watoto Wenu Sawa

Next
Next

Tujifunze Kushukuru