Mkono Mtupu Haulambwi

Simulizi
by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).
Mtu kama hana chochote, mfano mahitaji ya msingi nk., hawezi kuheshimiwa katika jamii. Huchekwa na kudharauliwa sana. Huonekana hana maana kwenye jamii yake. Anaweza akatoa ushauri wa aina yoyote lakini asisikilizwe. Kama binadamu yeyote, anaweza kutaka kumposa binti wa hapo mtaani/kijijini kwake na akakataliwa. Watu wanaweza wakamwambia bayana, “una nini wewe hata utake kumposa binti mrembo kama huyu”? Maneno haya huweza kumkatisha tamaa kijana anayekataliwa na mwisho yakamfanya asononeke na hata kupata msongo wa mawazo.
Binadamu tumepewa vipawa na karama tofauti. Ukubwa wa karama na vipawa pia hutofautiana. Utumiaji wa vipawa ama karama navyo hutofautiana mtu na mtu. Wengine huweza kutumia vipawa na karama zao kwa kujitengenezea maisha mazuri. Kuna baadhi ya watu hushindwa kutambua vipawa na karama walizo nazo na hivyo huishia kuishi maisha ya tabu, maisha yasiyo na matumaini. Watu wa aina hii ndio wanaweza kuwa kwenye kundi la “mkono mtupu haulambwi”.
Inatupasa, kama binadamu kuwa wabunifu katika maisha yetu. Kila mtu amepewa kipawa fulani na Mungu. Ni jukumu letu kutambua vipawa vyetu tulivyopewa na kuvitumia ipasavyo. Inatakiwa mikono yetu isiwe mitupu bali tuwe na chochote cha kutoa kwenye jamii zetu. Umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii kunamstahilisha mtu kupata heshima na kutambuliwa katika jamii yake. Hima kila mtu afanye kazi kwa bidii kwa kadri ya uwezo wake.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania