Tamaa Mbele, Mauti Nyuma

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha tunayoyaishi wanadamu lazima yawe na mwongozo au mwelekeo unaokupeleka kwenye malengo yenye tija, kwa mtu binafsi na hata kwa jamii inayokuzunguka. Kuna mambo yameshamiri sana siku hivi katika jamii yetu, hasa kwa vijana wetu ambao hupenda kuiga vitu ambavyo ni vya hatari katika maisha yao.
Ndoto zao ni kupata kipato au utajiri wa harakaharaka bila kujali ni kwa njia au jinsi gani. Ndoto hizi, mara nyingi, huwapeleka kwenye umauti na hata kufungwa jela.
Matukio mengi ya vijana wadogo wadogo, tena ya kusikitisha na kutisha ni yale ya kujiingiza kwenye biashara za dawa za kulevya, kwenye ukahaba, na kwenye hili wimbi jipya lilioanza kushamiri kwa kasi sana la “Panya Road”. Haya ni matokeo ya tamaa iliyowajaa ndani mwao kwa ajili ya kupata utajiri. Sote ni mashahidi kuwa hayo yote wanayoyafanya vijana wetu mwisho wake huwa ni mbaya sana, huwa hawafiki popote, huishia ama kifungoni ama kupata maradhi. Hali kadhalika wanaweza wakapigwa sana hadi kufikia hatua ya kuuawa, na hivyo kuleta hudhuni na masikitiko makubwa ndani ya familia na jamii kwa ujumla. Isitoshe, vitendo hivyo huleta aibu kubwa kuanzia familia husika na taifa kwa ujumla.
Cha kushangaza na kusikitisha zaidi, ni kwamba vijana wetu hawajifunzi kutokana na matukio mabaya ambayo yanawakuta wenzao. Wao wanachotaka na kuona mbele yao ni mafanikio tu ambayo hayana baraka yoyote ndani yake zaidi ya mauti na suluba na tabu tele baada ya hapo.
Kutokana na msemo huu wa busara, kama jamii, yatupasa kujifunza yafuatayo:
- Tuwalee watoto wetu katika misingi ya kuridhika na kile walichonacho. Kama wazazi, yatupasa kuwaambia watoto wetu ukweli kuhusu maisha, wasiweke tamaa mbele kwenye mambo ambayo hayana tija na ya hatari.
- Watoto waelimishwe ubaya wa kutafuta njia za mkato za kujipatia kipato au utajiri.
- Wazazi, tuwachunguze watoto wetu na kuzijua shughuli wanazofanya, tusingoje mpaka wanafikia hatua ya kufungwa ama kuuawa.
- Taifa na jamii kwa ujumla iwe na mikakati ya dhati ya kudhibiti matendo hayo maovu ya vijana. Ikiachwa hali hii kuendelea kwa kasi kama ilivyo sasa, inakuwa fedheha kubwa kwa nchi yetu ambayo inajulikana ulimwenguni kuwa ni nchi ya amani.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania