Kila Mchuma Janga, Hula na Kwao

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuchuma kitu, liwe tunda au hata mboga za majani ni sentensi inayoeleweka, maana hatima yake mboga ya majani au tunda lililochumwa ni kutayarishwa na kuliwa na watu. Lakini unaposema kuchuma janga haieleweki bila ufafanuzi zaidi. Msemo huu wa kila mchuma janga hula na wa kwao ina maana mtu anapopatikana na janga, ndugu zake, jamaa zake, watu wa ukoo wake, ndio watakaowajibika kumsaidia. Mfano, mtu akipata ajali na kuvunjika sehemu mbalimbali za mwili, akalazwa kwenye wodi ya mifupa, pengine mpaka kuja kupona inawezekana ikachukua mwaka au zaidi. Zile gharama za kwenda kumwona na kumpelekea chakula kila siku, gharama za matibabu nk. ndugu zake ndio watakaochangia. Hii ndio maana ya msemo huu.

Dunia kwa sasa imebadilika sana. Upendo haupo tena katika jamii. Watu wengi wanaonekana kutojali mfumo wa upendo uliokuwepo hapo zamani. Kuwajali wagonjwa kumeanza kuonekana ni mzigo kwa watu/ndugu na jamaa wengi. Wagonjwa wamekuwa hawajaliwi tena, kiasi kwamba wagonjwa wengine wanaweza wakaachwa mawodini bila huduma yoyote na wengine hata kufa na kuzikwa na manispaa kwa kukosa ndugu,
kitu ambacho zamani hakikuwepo na kilikuwa hakiwezekani asilani.

Pamoja na kwamba zamani tulikuwa hatuna mawasiliano ya haraka, bado mawasiliano ya mbali yaliweza kuwafikia wahusika, japo yalichukua muda mrefu. Mtu aliweza kutumwa na aliweza kumaliza hata wiki kupeleka taarifa ya ugonjwa wa ndugu yao. Cha msingi ni kwamba ndugu walipopata taarifa hizo walimkimbilia mgonjwa wao. Waliweza kuja na kitu chochote mikononi mwao, mathalani, fedha, mahindi ama chakula cha aina yoyote, majogoo au mitetea na hata mbuzi kutegemeana na uwezo na jinsi walivyoguswa na ugonjwa wa ndugu yao.

Lazima tujiulize, upendo wa zamani umekwenda wapi? Moyo wa kusaidiana umekwenda wapi? Hali hii ya ubinafsi tunayoina kushamiri kwa nguvu zote, imetoka wapi? Watu wamebakia na familia zao tu kusaidiana na siyo ndugu na jamaa kama ilivyokuwa zamani. Wana ukoo wako wapi?
Kwa nini watu wanakwepa kuyatelekeza majukumu yao ya kijamii ambayo ni ya msingi? Zimebaki familia peke yao kufanya kila kitu kwa ajili ya wapendwa wao, yatupasa tujiulize, KULIKONI?

Pengine zamani watu walikuwa hawaugui sana wala kupatwa na majanga mbalimbali kama ilivyo siku hizi. Je hii ni kwa sababu watu tulikuwa tunajaliana sana? Uko wapi upendo ule? Umekwenda wapi? Yatupasa tujiulize na kujaribu kuurudisha kwa nguvu zetu zote. Ni jukumu la kila mtu, jukumu la kila jamii na jukumu la taifa letu kushughulikia pengo hili, pengo ni kubwa sana na linaongezeka kila uchao.

.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Samaki Mmoja Akioza, Wote Wameoza?

Next
Next

Tamaa Mbele, Mauti Nyuma