Siri Ya Mtungi Aijuaye Kata

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mtungi ni chombo ambacho hutengenzwa kwa udongo wa mfinyazi halafu huchomwa kwa moto ili kuimarisha ubora wake na kuzuia kupasuka kiurahisi. Mtungi hutumika sana katika jamii yetu kuhifadhia maji ili yapate ubaridi.

Makabila mengi hapa Tanzania yana uzoefu wa chombo hicho na mara nyingi kuteka maji kwenye mtungi wanatumia kata. Hiki chombo kiitwacho kata hutengenezwa kwa kutumia kopo na mti mrefu huchomekwa kwenye hilo kopo ili maji yaweze kuchotwa kwenye mtungi bila kuyachafua. Tunaweza kusema kuwa kwa vile kata inatumika kuchota maji kwenye mtungi, yenyewe ndiyo inabeba siri zote za mtungi, yenyewe inajua kama maji kwenye mtungi yamejaa au yapo nusu au yana matope pale yanaposhindikana kuchoteka. Hali kadhalika kata ndio inayoweza kujua kama maji yamekwisha ama la. Kwa hakika, kata inabeba siri nzito.

Habari ya mtungi na kata inatupa picha kamili ya maisha yetu ya kila siku. Familia nyingi zinaishi kwa malezi tofauti tofauti na siri za humo ndani zinajulikana mpaka mtu wa kutoka nje awe amekaa pale kwa muda wa siku mbili tatu ndipo atakapogundua mazuri ama mabaya ya humo ndani. Huyo mtu wa kutoka nje ni kama kata ambayo inajua siri ya mtungi.

Kuna matukio mengi yanafanyika sehemu mbalimbali ambayo siyo sahihi. Matukio hayo mabaya huwa ni siri ya kila nyumba/familia, yanaweza kufichuliwa na mtu kutoka sehemu nyingine nje ya familia husika. Endapo mambo hayo hayatafichuliwa yataendelea tu na hatimaye, kuwa ya kawaida kabisa.

Kuna wakati hiyo siri inaweza kujulikana kama italeta matokeo hasi. Kwa mfano kama kwenye familia kikitokea kitu kibaya kati ya mwanafamilia mmoja na mwingine, watu wa nje ya familia hawataweza kujua kinachoendelea ndani ya familia ile.

Hapo tumeona kwamba kata ni chombo kidogo sana, kinatunza siri ya mtungi. Yatupasa tukumbuke kuwa tunapofanya matukio makubwa kwa siri na watoto wanaona, tusiwadharau, wanaweza kukuumbua hadharani. Hali kadhalika, wanaweza wakakunyamazia ama kukaa kimya na kutosema matukio yako uliyoyafanya. Kata ni chombo kidogo lakini kinahifadhi siri kubwa sana ambazo wengine hawazijui.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Wanawake Tunaweza

Next
Next

Kuomba Msaada, Kukopa Na Kurudia Makosa Sio Vibaya