Wanawake Tunaweza

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Nikianzia tangu zamani wanawake wamekuwa muhimili mkubwa wa familia zao. Huko vijijini unakuta baba ana wake ni 5/6 au zaidi. Wanawake hawa ambao wameolewa kwa mume mmoja ni kama vitendea kazi vya mume wao. Mara nyingi wanaume wengi huwa hatunzi familia zao. Kazi zao kubwa ni kula raha na kulewa pombe wakati wote, huku akijipongeza kuwa ana ‘watumishi’ wake nyumbani. Wakirudi nyumbani wanataka wakute chakula kipo hata bila kujali chakula hicho kinatoka wapi.
Wakati mwingi akina mama wamekuwa ni watunza familia bila kuwezeshwa na waume zao ambao ni baba za watoto wao. Bila kusaidiwa na waume zao, watoto wanakula, wanaenda shule na hata wakiumwa wanapatiwa matibabu.
Kuna mifano hai ya akina mama waliofiwa na waume na kuwa wajane. Kabla ya kufiwa, akina mama hawa walikuwa wakiishi maisha magumu na ya shida. Hali kadhalika, walikuwa wakiishi maisha ya manyanyaso. Cha kushangaza, baada ya waume zao kufa, wajane hawa hawakutetereka bali walisimama imara na kuendelea kutafuta maisha mazuri kwa ajili ya familia zao. Yote hii inawezekana kwa sababu wanawake ni jasiri, wavumilivu, na ni wathubutu wazuri sana.
Na hata makanisani wanawake ni jeshi kubwa. Yaani ndio wanaofanya kanisa linasonga mbele, maana umoja wao ni wa nguvu sana. Ninachotaka tujifunze hapa ni kwamba wanawake wana uwezo mkubwa sana.
Kwa wasomaji wa andiko hili, kama wewe ni mwanamke tunakushauri ujivune kuumbwa mwanamke maana hizi sifa za ujasiri, uthubutu, uvumilivu, uhodari zipo ndani yako tangu ulipokuwa tumboni mwa mama yako. Endapo utazingatia na kukaa vizuri katika nafasi yako kama mama utakula mema ya nchi. Kwa wasomaji wanaume hali kadhalika, tunataka mjifunze kuwa baba wazuri wa familia na siyo kuacha mizigo yote kwa wake zenu. Kila mtu, awe mume ama mke ana sehemu yake ya kufanya katika maisha yetu ya kila siku.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania