Nahodha Wengi, Chombo Huenda Mrama

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ni maisha yetu ya kila siku uwe nyumbani, maeneo ya biashara, maofisini, ama kwenye taasisi mbalimbali lazima utakutana na huu msemo. Kwa kawaida, Kiongozi huchaguliwa na huwa ni mmoja tu na huyo ndiye huwa na kauli ya mwisho ya kutoa maamuzi. Ikiwa kila mtu atatoa ya kwake hapatakuwa na amani wala maelewano katika utendaji.
Katika hali ya ubinadamu mara nyingi kwenye maeneo mengi kuna baadhi ya watu huwa hawaridhiki kuona fulani anaongoza. Utakuta wanaanza makundi makundi na kuingilia majukumu ya kiongozi wao na mwisho huharibu mwenendo mzima wa hiyo Taasisi au ofisi husika.
Tumeshuhudia migogoro mingi kwenye makapuni au ofisi mbalimbali. Wafanyakazi wengine huwaingilia mabosi zao na kuvuruga kabisa mwenendo mzima wa uendeshaji wa hizo ofisi. Wakati mwingine wafanyakazi hukaa na kupanga safu zao. Mara nyingine mgawanyo huu hupelekea hata kufanya migomo ambayo wakati mwingine husababisha vurugu hata kuharibu mali za ofisi au kampuni.
Ni jambo jema ambalo linakubaliwa katika maisha yetu kuwa na uongozi ambao utasimamia mambo mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Uongozi unaanzia kwenye ngazi ya familia na unaenda moja kwa hadi kwenye sehemu zetu za kazi mbalimbali kwenye jamii.
Msemo huu unatufundisha kwamba yatupasa kuheshimu mamlaka ambayo iko juu yetu. Bila kuwa na kiongozi mambo yataenda hovyo hovyo na wakati mwingine mtashindwa kufikia malengo mliyojiwekea.
Kwanza siyo utaratibu mzuri kuwa kila mtu afanye anachokitaka, au atoe maamuzi yake. Mwisho wake ni kudharauliana na kukosekana kwa maelewano na vurugu katika sehemu ya kazi.
Katika hali ya vurugu na utengano, hatajulikana mkubwa ni nani na mdogo ni nani! Katika hali hii, mwisho wake huwa ni mbaya. Tujiepushe na mambo yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani. Msemo huu unafanana na ule wa “Wapishi Wengi, Huharibu Mchuzi”.
.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania