Leo Kwako Kesho Kwa Mwenzio

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mara nyingi tuna tumia msemo kwa kufundisha upendo. Tunashauriwa kutopenda kufurahia matatizo ya wenzetu. Pengine unaona ni sahihi kufurahia matatizo yao kwa sababu watu hao waliisha kuudhi, kukukosea na mkatofautiana kwa jambo fulani. Wengi tuna hiyo tabia, kwa vile mlipishana wakati fulani, ukisikia tu mwenzio yamemkuta unaanza kufurahi na kusema sema kwa watu, “eeh nilijua tu yatakuwa hivyo.” Utaendelea kusema maneno mengi yasiyokuwa ya busara.
Kumbuka kwamba sisi wote tunaishi hapa duniani kama wasafiri, wapita njia, na kwamba hakuna atakayeishi milele. Hivyo ni vema tukaishi kwa upendo na kusaidiana. Upendo huu usambazwe hata kwa wale waliokuumiza. Kamwe usiwaweke moyoni maudhi yao. Mwenzio anapopatwa na janga tumia BUSARA ya kumliwaza, mtie moyo, mpe matumaini kwa yale anayopitia na sio kuzidi kumuumiza kwani hilo sio jambo jema hata kidogo. Na unapofanya hivyo ndio tunaposema "leo kwako, kesho kwa mwenzio". Au kwa maneno mengine usilipize ubaya/kisasi kwa mwenzio maana hujui kesho huyo huyo ndio utamkuta mahali unapohitaji huduma muhimu na unaweza ukakuta hakuna mtu mwingine atakayeweza kukusaidia zaidi ya huyo unayemuona kuwa ni hasidi yako. Haifai kabisa. Tuwe waungwana na wastaarabu. Busara zitawale.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania