Kilichoanguka Kitainuka Tena

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha ya hapa duniani ni mzunguko ambao kila binadamu aliye chini ya jua hili, lazima apitiwe kwenye mzunguko huo. Maisha sio barabara ya lami.

Kuna mtu mmoja ambaye alikuwa na hali ngumu sana kimaisha. Alikuwa anategemea asaidiwe na watu, hususani, ndugu, lakini hakuna ndugu yeyote aliyeweza kujitokeza na kufanya hivyo.

Jamaa huyu aliihangaikia sana elimu yake na kama waswahili wasemavyo, ‘Mungu si Athuman,’ pamoja na kuhangaika na misukosuko yote ya maisha, jamaa alifanikiwa kusoma hadi kupata shahada. Elimu hii ilimuwezesha kuajiriwa kwenye nafasi nzuri sana serikalini. Kwa hakika, jina lake lilitukuka kwa mafanikio hayo.

Cha ajabu ni kwamba, watu ambao walikuwa wanamnyanyasa na kumcheka huko nyuma, ndio walikuwa wa kwanza kabisa kwenda kuomba msaada kwake. Hawakuwa na aibu yoyote, walikuwa wamesahau yote ya nyuma. Hawakukumbuka kabisa yale waliyokuwa wamemtendea na kumfanyia hapo awali.

Fundisho letu kwetu sote ni kwamba tusimnyanyase mtu yeyote katika maisha yetu hapa duniani. Unapojiona kuwa wewe unacho ama kujiona kuwa wewe ni bora kuliko wahangaikao, yakupasa ukumbuke kuwa dunia yetu ni mviringo. Mambo yanaweza kukubadilikia mara moja na ukajikuta uko katika hali ambayo hukuitegemea. Na kwa yule ambaye anajiona kuwa hajiwezi, yampasa asikate tamaa kwani mambo yake yanaweza kubadilika na kuwa mazuri hadi watu wakashangaa na kuona aibu kwa yale waliyomtendea, ya kumcheka kutokana na hali yake ya kutojiweza. Sote tunaijua jana na leo, lakini ya kesho hayako ndani ya uelewa wetu. Hivyo sote hatujui kesho yetu itakuwaje.

Tujifunze kuwa ‘Kinachoanguka leo, Kesho Kitainuka’ na kwamba, wewe na mimi tunaweza tukawa watu wa kwanza kumfuata yule tuliyemdharau. Yatupasa tukumbuke kuwa ‘Dunia ni duara, inazunguka’. Wahenga pia walinena, ‘dunia ni tambara bovu’, na sote tunaipitia ikiwa hivyo ilivyo.

TUHESHIMIANE, TUSAIDIANE na TUNYANYUANE pale inapowezekana kwani sote ni wamoja. 🙏🏽🙏🏽

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Zawadi Haina Udogo

Next
Next

Hakuna Mtu Anayejua Kila Kitu