Zawadi Haina Udogo

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Zawadi ni chochote, unapopewa pokea kwa furaha. Kuna baadhi ya watu huwa hawalitambui hili. Mathalani, mtu akipewa zawadi, kwanza anaiangalia uzuri na ukubwa wake, hata na gharama ya kununulia ile zawadi angependa kuijua . Endapo utaona hiyo zawadi haikidhi vigezo vyako, utaidharau kwa kunong'onanong'ona vineno pembeni. Unaweza hata kudiriki kusema, “Oh, zawadi gani hii jamani, siyo nzuri, sijui amenionaje, mbona ananidharau sana”.

Huku ni kukosa shukrani. Yakupasa uthamini muda na gharama alizotumia kukuletea hiyo zaidi. Isitoshe, kilichomsukuma huyo mtoa zawadi ni upendo mkubwa aliokuwa nao kwako mpokeaji. Ni vema ukajiuliza pia, kwa nini upewe wewe zawadi na asipewe mtu mwingine? Ingekupasa uone na kutambua kuwa huo ni upendo uliotukuka dhidi yako.

Zawadi haikosolewi, zawadi inathaminiwa. Kukosoa zawadi unayopewa sio ustaarabu hata kidogo. Ni kukosa ubinadamu na heshima kwa mtoaji. Hali kadhalika, kusema sema vineno pembeni juu ya zawadi uliyopewa ni utovu mkubwa sana wa nidhamu. Haipendezi kabisa.

Cha msingi, tuwe na uungwana na moyo wa kutosheka na kuridhika na chochote tupewacho. Kumbuka kuwa zawadi ni zawadi, si haki yako na kwamba akupaye kagharamia. Hata kama haikufurahishi machoni pako na pengine unaona kuwa ni kidogo sana, huna budi kumshukuru mtoaji. Usiposhukuru kidogo hata kikubwa hutaweza kushukuru. Shukurani yaanza na vitu vidogo na hasa pale inapokuwa ni zawadi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Sio Kila Rafiki Ni Wa Kweli

Next
Next

Kilichoanguka Kitainuka Tena