Faida Na Hasara Za Kuiga

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wengi tumezoea na tunapenda kuiga mambo ya watu wengine na hata pengine kuifanya tabia hiyo kuwa mtindo/taratibu za maisha yetu hapa duniani. Lakini katika kuiga huko ni lazima kuwa waangalifu sana, siyo kuiga kila kitu. Mfano, akina mama wengi hupenda kuiga mitindo ya mavazi, kusuka nywele na hata biashara. Wengine huiga kiushindani tu, na si vinginevyo. Izingatiwe kuwa kuiga kiushindani sio sahihi kabisa.
Wengine hata wamediriki kulazimisha hata watoto wao waolewe ama waoe kutoka familia za kitajiri. Yote hii hufanyika katika jitihada za kuiga familia nyingine. Ukweli ni kwamba mambo haya hayaigwi, bali huweza tokea kutokana na kibali kutoka kwa Muumba.
Kuna ushuhuda ambao inafaa utolewe ili kutia uzito kwenye mazungumzo haya. Niliishi na mwanamke mwenzangu wakati nafanya kazi mikoani. Tuliishi nyumba moja na tulikuwa tunafanya kazi kwenye shirika moja. Huyu mama alipenda sana kuiga kila nifanyacho. Ilitokea kuwa kila nilichokuwa ninanunua, alijitahidi na yeye awe nacho. Kwa stahili hii ya maisha ya kuigaiga kila kitu, ilimlazimu atumie kila njia, hata kukopa ili aweze kupata. Matokeo yake alijikuta akiwa na madeni mengi na hivyo kukosa amani moyoni.
Mwanzoni nilifikiri labda alikuwa na wivu lakini baadaye niligundua kuwa ilikuwa ni tabia yake kwa kila mtu. Kwa wengine alikuwa anaiga wanachofanya, kwa mfano mtu akihadithia jambo fulani, kesho yake yeye atalisimulia jambo hilo kama vile la kwake. Yaani huo ndio ulikuwa mtindo wa maisha yake.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuiga ni jambo jema kama linaleta faida kimaendeleo. Kuna watu wengi ambao wamefanikiwa katika maisha yao kwa kuiga maendeleo. Lakini siyo busara kabisa kama mtu anaiga kwa ushabiki, mashindano, ili afanane na fulani. Mara nyingi, mwisho wake huwa siyo mzuri kwani unaweza kujikuta unakuwa na matumizi makubwa ambayo hayaendani na mahesabu uliyonayo. Mwisho utajikuta unalazimika kukopa na kufikia madeni ambayo huna uwezo wa kuyalipa. Ukifikia hapo maisha yako yatakuwa hayana amani wala furaha. Waswahili husema, ‘Tamaa Mbele, Mauti Nyuma.’
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania