Ili Kufanikiwa Ni Lazima Uhame

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Watu wengi tumezoea sana kuishi kwa kutegemea leo. Mara nyingi wengi hujifariji na hudiriki hata kusema, “Ya kesho anayajua Mungu.”

Usemi huo juu unatufundisha namna unavyoweza kubadilisha mpangilio wako wa maisha hapa duniani. Tunashauriwa kuwa ukitaka kutoka kimaisha yakupasa kuondokana na tabia ya kufanya mambo yako kwa mazoea. Ni jambo lisilokuwa na ubishi kuwa maisha ya hapa mjini hutofautiana sana kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine. Mathalani, maisha ya eneo moja yanatofautiana na eneo jingine. Kuna sehemu unaweza kuishi kwa Sh.. 500 au kwa Sh. 1,000. Mahali kama hapo huwezi kubadilika au kuendelea maana utakuwa unaridhika na kuendana na hali halisi ya mahali hapo.

Lakini kuna sehemu nyingine maisha yanaweza kukubadilisha kutokana na hali halisi ya watu wanavyoishi. Katika hali ya kawaida, itakulazimu kuwauliza wenyeji wako jinsi wanavyoishi mahali hapo ili na wewe uweze kutafuta mbinu za kukuwezesha kuishi hapo. Ukifikia hatua hiyo ya kuulizia maisha na taratibu za kuishi hapo, huo ndio utakuwa mwanzo wa kubadili mfumo wa maisha yako. Itakuwa ni tofauti na maisha ya kule ulikotoka. Utabaki na ushuhuda wa kule ulikotoka, jinsi maisha yalivyokuwa na mengine mengi. Huko utakutana na watu ambao mipango yao ni ya wiki au mwezi, mipango inayoangalia mbele tofauti na mipango ya siku moja moja tu ambayo ulikuwa umeizoea. Ukiwa kama mgeni kwenye sehemu hiyo, itakupasa kubadilisha maisha yako ya huko nyuma ili kuweza kuishi hapo mahali papya. Hapa ndipo utakapoondokana na maisha yako ya nyuma na huo ndio utakuwa mwanzo wa kusonga mbele.

Yatupasa tusiishi kwa mazoea ya kuridhika. Tuishi kwa kujua kuwa kesho ni siku nyingine na ina mambo mengine na mapya. Usiogope kuthubutu kwa lolote, maisha ndivyo yalivyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Chagua Mamboa Ya Kujifunza Na Kutafakari

Next
Next

Chezea Mshahara, Usichezee Kazi