Mtaji Wa Maskini Ni Nguvu Zake Mwenyewe

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Umasikini ni hali duni ya maisha inayompelekea mtu ashindwe kukidhi mahitaji yake ya msingi. Mahitaji hayo ni kama vile chakula, mavazi, malazi na mengine mengi yanayoweza kumfanya mtu ajisikie yuko barabara na kuyaona maisha yake kuwa ya thamani. 

Mara nyingi, umaskini mwingine ni wa kujitakia. Mathalani, unaweza ukamuona mtu/kijana ambaye muonekano wake ni wakuvutia, na ana afya njema. Kijana huyu anaweza akaamka asubuhi na asifanye chochote zaidi ya kuzurura tu. Utamsikia akilalamika kuwa maisha ni magumu na pia haoni sababu ya kuishi. Atalalamika kuwa anashindwa kupata hata fedha kidogo kwa ajili ya matumizi yake madogo madogo. Unaweza ukabaki ukijiuliza kama huyo kijana anamaanisha maneno yake hayo. Utatamani umuulize kama ana akili timamu ama la. Utatamani kumuuliza jinsi anavyozitumia nguvu zake kwani ukimuangalia anaonekana kuwa ni bonge la mtu ambaye hawezi kukosa kazi yoyote, hata ya kubeba mizigo kwenye masoko makubwa, hususani, yale ya jumla. Kwa hakika utajiuliza, ni kwa nini asiyatumie hayo maguvu anayoonekana kuwa nayo katika kufanya kazi ili apate mahitaji yake? 

Watu wa aina hii wanaweza kufanya kazi na wakaboresha maisha yao kwa kutumia fursa mbalimbali zilizopo. Yatupasa kila mmoja wetu, hususan vijana tuache kunung’unika kila uchao kuhusu ugumu wa maisha. Kila mmoja amepewa mtaji ambao ni nguvu zake mwenyewe. Nguvu hizo zitumike kwa faida na maendeleo yetu. Mtaji wa Masikini mi nguvu zake mwenyewe.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Sio Kila Wakati Mume Ana Makosa

Next
Next

Chagua Mamboa Ya Kujifunza Na Kutafakari