Muacha Asili Ni Sawa Na Mtumwa

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).

‘Muacha asili’ ni mtu ambaye ameacha ama hafuati kabisa mila na desturi za kule atokako. ‘Mtumwa’ ni mtu yule anayemilikiwa na mtu mwingine na analazimika amtumikie. Mtu wa namna hiyo mara nyingi huwa hana uwezo wala nguvu ya kujitambua na wala kujua ama kuikubali asili yake ama chimbuko lake. Mtu wa namna hii huweza dharauliwa sana kwa kukosa kujua chimbuko lake.

Kwa hiyo mtu ambaye anadharau au ameacha mila na desturi za kwao huweza linganishwa na mtumwa. Mtu huyu anakosa kitambulisho cha kumuonyesha yeye ni nani. Mathalani, ikiwa ameiga mila na desturi za watu wengine, ni rahisi watu wakamchanganya na kumdhania kuwa yeye ni kama hao watu wenye mila aliyoiiga. Endapo mila ama tabia hiyo ni mbaya/mbovu basi na yeye atahesabika kwenye ubovu huo na hivyo kukosa thamani kwenye jamii inayomzunguka.

Tumeona watu wengi, hususan vijana kupenda kuiga iga mila na tabia za watu kutoka magharibi. Kwa kuiga watu wa magharibi, pengine namna wanavyotembea , wanavyoongea, wanavyovaa, n.k. wanajiona kuwa wameendelea sana. Kwa kuiga taratibu na tabia za watu wengine
mhusika anakuwa hana tofauti na mtumwa kwa sababu mtumwa kwa kutoweza kuijua asili yake, huiga mila na desturi za bwana zake wanaommiliki.

Msemo huo hutumiwa kuwahimiza watu wajiheshimu, wasidharau mila na desturi zao hata kama watu wengine wanaziona si kitu sms si nzuri. Kwa kufanya hivyo, ndivyo watu wengine wataweza kukuthamini na kukuheshimu. Yatupasa tulinde na kuheshimu mila na desturi zetu kwa ajili ya utambulisho wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Mwenda Kasi, Mngoje Achoke

Next
Next

Nyakati Ngumu Hutengeneza Watu Imara