Eti Mtoto Wa Kike Ni Nyanya, Ikikaa Sana Itaoza

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Usemi huu unapingwa sana na watu wote wenye busara na akili timamu. Kwanza siyo sahihi hata kidogo kulinganisha binadamu na nyanya mbovu ama kitu chochote kile. Tunapoangalia suala la malezi ya mtoto wa kike tunaona kuwa anahitaji uangalizi wa hali ya juu zaidi kuliko mtoto wa kiume. Hii ni kutokana na maumbile yake, pia na nafasi ya mwanamke katika jamii, nafasi ya kuonewa. Kutokana na ukweli huo, tunaamini kuwa inampasa mtoto wa kike afundishwe katika kila hatua anayopitia ili ajue jinsi ya kujilinda na yote yatakayofuata katika kila hatua ya makuzi yake.
Usemi wa "Mtoto wa kike nyanya mbovu ikikaa sana itaoza", umekuwa ukitumika sana hasa kwa baadhi ya jamii ya wafugaji na wale ambao bado wanaendeleza mila potofu. Ulinganisho wa nyanya mbovu na mtoto wa kike siyo sahihi hata kidogo. Wanaotumia usemi huu ni wale wanaoamini kuwa mtoto wa kike asipoolewa katika umri mdogo anakosa thamani. Fikra hii ni kinyume na ukweli kwani akiolewa mapema kuna madhara yanayoweza kumpata wakati wa uja uzito na hata kujifungua kwake kunakuwa ni hatari kubwa. Baadhi ya jamii hizo na wenye mila potofu huona kuwa hakuna haja ya kuwapa watoto wao wa kike haki ya elimu. Wakati mwingine huwasomesha hadi kumaliza elimu ya shule ya msingi tu.
Mara nyingine nyingine wazazi hata hudiriki kuwashawishi watoto wafanye vibaya mitihani yao ya kumaliza elimu ya shule ya msingi ili wakaolewe. Mtoto wa kike kusoma hadi Chuo Kikuu huonekana kuwa ni wazo baya kwani litawapotezea muda, umri utakuwa umekwenda sana. Kisingizio kikubwa eti ni binti akiwa na umri mkubwa mara nyingi huwa ni shida kupata mchumba, hii si kweli.
Fikra hizi ni potofu na pia ni za uonevu kabisa kwa sababu kwa kawaida, kijana anapomaliza chuo kikuu anaweza kuwa na umri wa miaka 22 hadi 27 ambao bado unakuwa ni umri muafaka wa kuolewa. Lakini pia ikumbukwe kuwa maendeleo hayaletwi na vijana wa kiume pekee yao. Uzoefu unaonyesha kuwa siku hizi, vijana wa kike kwa dunia ya leo wanaleta maendeleo makubwa zaidi kuliko vijana wa kiume. Ule usemi unaosema kuwa, “Ukimsomesha mwanamke unasomesha jamii nzima” unasisitiza ukweli huu.
Yatupasa tuwape haki ya elimu watoto wetu wote bila kujali jinsia zao. Watoto wote, awe mvulana ama msichana, ndio tegemeo la maendeleo kwa taifa letu. Hebu tuache ubaguzi usiokuwa na maana kwa maendeleo yetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania