Penye Riziki Hapakosi Fitina

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha yetu ya hapa duniani kwa sehemu kubwa yametawaliwa na wivu kutokana na roho zetu mbaya. Ni watu wachache tu ambao wanaweza kukupongeza kwa dhati katika mafanikio yako. Walio wengi hupenda kuona mtu anaishi kwa shida na kwa tabu, eti hiyo ndio huwa ni furaha yao kubwa. Watu kama hawa huwa hawako tayari kukusaidia ama kukutoa kwenye hali ya dhiki ambayo unaweza kuwa nayo. Wengine hufikia hata hatua ya kukutenga na kuwa mbali na wewe, kwa vile tu hali yako ni duni.
Lakini tukumbuke kwamba Mungu amemuumba mwanadamu ili afurahie maisha aliyompa hapa duniani. Kwa vile Mungu wetu hana choyo, ipo siku atakuinua na kukutoa kwenye hiyo hali ya dhiki. Mungu akikuinua basi ndipo na vita dhidi yako vitainuka kwa nguvu zote. Binadamu hawapendi wenzao wainuke kwa maana wanajua sasa na wewe utakuja kuwa kama wao.
Ajali ya ndege ilimuibua kijana mdogo Majaliwa ambaye alitumika na Mungu kuokoa watu, hali ambayo ilikuwa karibu imsababishie na yeye mwenyewe umauti. Ilikuwa naye afe katika jitihada za kuwaokoa binadamu wenzake ambao hana hata udugu nao. Ni huruma tu ya Majaliwa iliyotawaliwa na utu wake.
Utashangaa sasa watu wameanza kubeza kile kilichofanywa na serikali. Kuna wanaoona kwamba hakustahili, hii ni kutokana na vile alivyozawadiwa na serikali. Pengine kama sio Majaliwa kujitoa mhanga, watu wengi zaidi wangelikufa. Tukumbuke kuwa kazi yake ya kuokoa watu nusura na yeye afe, alijikuta yuko chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kutoswa na maji.
Binadamu kweli hatuna shukurani wala fadhila. Lakini hiyo yote ni mioyo iliyojaa chuki na nda, hatupendi wenzetu wafanyiwe ama walipwe mema kwa mazuri wanayofanya. Tunapenda kuona wenzetu wanahangaika na kwa kufanya hivyo, nafsi zetu hufurahi. Roho zetu zimejaa maneno ya ‘kwa nini’? Pengine tungependa kumuona Majaliwa akibakia pale mwaloni, akibangaiza na dagaa zake. Ni roho mbaya zilizokithiri.m ambazo zinatakiwa kulaaniwa. Lakini tujiulize, kwani mwenzio akihangaika na kupata tabu, wewe unapata nini?
Roho za ‘korosho’ hazifai. Yatupasa tuondokane na roho hizo kwani hazijengi zaidi ya kubomoa. Mungu humuangalia kila mtu kwa wakati wake. Sisi sote ni viumbe wake hivyo tupendane na tusaidiane kama binadamu tuliopo hapa duniani. Tujifunze kusherehekea mafanikio ya wenzetu, kwa kufanya hivyo tutakuwa tunayakaribisha mafanikio ya kwetu ambayo yako njiani, yanakuja. Tuwe na subira 🙏🏽
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania