Wengine Hupanda Mbegu Kupitia Wewe

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Sio kila anayetoa msaada kwenye maisha yako, anatarajia kupata kitu au faida ya kile anachofanya kwenye maisha yako. Kuna watu ambao furaha yao ni kuona unafanikiwa. Wao hufurahi pale wanapoona wanakuwa sehemu ya kusaidia watu ili wawe vile ambavyo Mungu amekusudia wawe.
Jitahidi sana usiwadharau watu hao, usiwaone kuwa ni watu wa kawaida kwako. Uwaone kuwa ni watu muhimu kwenye maisha yako. Waone kama watu wenye malengo, wana maono ya mbali.
Kuna watu wengine wakiona kile umebeba ndani yako wanakuwa radhi kulala njaa ili wakuinue wewe. Watu hawa huwa radhi hata kuvunja ratiba zao za kazi ili wapate muda wa kukuombea wewe.
Usipojifunza kuthamini machozi ya wanaokesha usiku, huku wakilia, wakifanya maombi kwa ajili yako, wakitoa mali zao kwa ajili ya huduma yako, kwa ajili ya masomo yako, na kwa ajili ya watoto wako, wewe utakuwa si binadamu wa kawaida. Yakupasa utambue kuwa kuna gharama, jiandae kuilipa kesho. Siyo kwamba huyo mtu ana muda mwingi sana wa kupoteza juu yako, ama ana mali nyingi sana na hana mahali pa kupeleka. La hasha. Inakupasa ujue kuwa anafanya hivyo kwa sababu kuna mbegu anaamini anaipanda, sio kwako, tu, bali hata mbele za Mungu, anakuwa anamkopesha Bwana. Mungu wetu hukopesheka, naye pia hurudisha kwa malipo mazuri sana. Tuwe na imani, tupande mbegu zetu ili baadaye tuweze kuvuna mema.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania