Kama Unapenda Sketi Za Shule, Mshonee Mkeo

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Wengi huuchukulia msemo huu kama utani na pia wa kuchekesha. Mara nyingi tunaona maandishi haya kwenye malori ama bajaji. Kusema kweli kwa upande moja maneno haya yanachekesha lakini kwa upande mwingine yanaweza yakamfanya mtu atafakari kiundani zaidi maana yake.  

Msemo huu unakuja baada ya kuona maadili ya watu, hususani baadhi ya wanaume yameporomoka. Kwa kawaida, waungwana wanatakiwa kuwathamini na kuwajali watoto wa wenzao. Lakini yanayotokea siku hizi, yanawauma na kuwaliza wazazi wengi pamoja na taifa kwa ujumla. 

Serikali ina upendeleo wa hali ya juu kwa mtoto wa kike, hususan, kielimu. Inasikitisha kuona kuwa, pamoja na jitihada hizo za Serikali za kumkomboa mtoto wa kike kielimu, kuna watu wasio na mapenzi mema na mabinti hao. Wabaya hao wamekuja na mbinu mbalimbali za kuwarubuni na kuharibu maono yao na hata kuharibu malengo ya Serikali. Ukichunguza sana ni kitu kidogo sana kinacho mponza binti mpaka anaharibu malengo yake. Inaweza kuwa shilingi 500 tu ambayo inamvuruga binti na hata kusahau kabisa malengo yake. Swali la kujiuliza hasa ni kitu gani kinamvutia mwanaume mzima kumfuata na kumlaghai mtoto ambaye anaweza kuwa sawa na binti yake au hata mjukuu wake? Je, wanaume hao, pengine wanawafuata hao mabinti kwa sababu wanapenda sketi zao? 

Ndio maana watu wamekuwa wakisema kwa mafumbo kuwa kama wanaume hao wanapenda sketi za mabinti hao basi wawashonee wake zao ili watulize mihemuko yao. Wanaaswa kuwa wasiwaharibie mabinti zetu malengo ya maisha yao ya mbeleni. Tunatoa ushauri kwa wanaume wenye tabia za kutamani na kupenda kuparamia sketi, wawashonee wake zao sketi zinazofanana na hizo wanazozitamani. Wawaache mabinti zetu ili waweze kutimiza malengo yao. Yatupasa tukumbuke kuwa, binti wa mwenzio ni binti yako hivyo mpe heshima na haki anazostahili, haki ya kumaliza masomo yake pamoja na haki ya kuishi kama mtoto. Elimu ya mtoto wa kike ni muhimu sana kwa taifa letu. Ule usemi wa: “Ukimuelimisha mwanamke, umeelimisha ulimwengu”, una maana sana kwa kila mtu. Kama tatizo la wanaume wenye tabia hii ni sketi za mabinti zetu, basi tunawaomba na kuwashauri kuwa kuanzia leo, wawashonee wake zao wapendwa sketi ili waweze kutunza ndoa zao. 

Mtoto wa mwenzio ni wako.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Unachokikataa Leo, Kinaweza Kukufaa Kesho

Next
Next

Wengine Hupanda Mbegu Kupitia Wewe