Fanya Maamuzi Kwa Mafanikio Yako

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Binadamu yeyote ana uwezo wa kufanikiwa kama akifanya maamuzi, kwani uwezo wa kufanikiwa uko ndani yake. Tatizo kubwa linalowapata wengi ni kufanya maamuzi. Tupo wengi tu ambao tokea mwezi wa Januari, tulijiwekea mipango mingi sana ya kufanya, lakini hakuna tulichotekeleza hata kimoja. Hii haimaamishi kuwa hatuna uwezo, shida kubwa ipo kwenye kufanya maamuzi. Tunatumia muda mwingi kuwaza jinsi itakavyokuwa, ama jinsi ya kufanya. Tunaendelea kujiuliza maswali hayo mpaka mwisho mwaka unaisha ukiwa hujafanya lolote. 

Matokeo yake hakuna unachopata pamoja na mipango yako mizuri uliyokuwa nayo. Kwa upande moja, inakuwa ni aibu kwa kutofanikiwa kwako wakati ulikuwa na mipango mizuri tu. Hukuweza kufanya lolote, wakati uwezo unao, nguvu unazo na hata mamlaka unayo. Unajiuliza sababu za kuwa hivyo. Unajikuta uko njia panda. Tatizo lako kubwa ni kushindwa kufanya maamuzi, na pengine bado hautaki ama hujaamua kuanza kufanya maamuzi. Wanaweza wakaja watu hapo hapo ulipo, wao wakafanya maamuzi na wakakuacha hapo hapo ulipo. Badilika! 

Lakini hujachelewa. Weka nia thabiti kwani waswahili husema, ‘Penye Nia Pana Njia’. Hujachelewa, anza sasa. Pitia mipango yako uliyokuwa nayo na anza kuitekeleza SASA kwa vitendo. Acha woga, acha hofu, jiamini. Amua, liwalo na liwe mbele kwa mbele ... utafanikiwa tu kwa uwezo wake aliyekupa hilo wazo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Usichezee Kazi, Chezea Mshahara

Next
Next

Chapa Kazi, Sio Mkeo