Usichezee Kazi, Chezea Mshahara

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mambo mengi yamebadilika sana tangu ulimwengu wa Sayansi na Tekinolojia kuzidi kupanuka katika ulimwengu wa leo. Jambo hili nimelishuhudia mimi mwenyewe kabla sijastahafu. Sisi wakati tunaajiriwa tulikuwa hatujui kutumia kompyuta wala hatukuwa na simu za mkononi. Tukiingia ofisini ni kuangalia mezani pako pana mafaili gani ya kuyashughulikia na mengineyo. 

Lakini jinsi utandawazi unavyozidi kupanuka, mambo mengi yameanza kupotea, hasa ufanisi katika utendaji kazi. Kabla sijastahafu niliwapokea waajiriwa wapya kutoka Chuo cha Kilimo SUA. Waajiwa wapya hawa walikuwa wakifika ofisini, wao ni kuongea na simu tu, ikifika saa 4 wanaenda kunywa chai. Wakirudi kutoka kwenye chai, wataanza kukumbushana ya huko kwanza na ndipo wataanza kuangalia mafaili. Nilikuwa najiuliza hivi, kizazi chetu kikiondoka, hizi kazi zitakuwa zinafanyika kweli? 

Kazi zenyewe za siku hizi, siyo kama ilivyokuwa kwetu sisi zamani. Kazi zilikuwa zinatungojea, tukimaliza chuo tu zinakuwepo tayari kwa ajili yetu. Tofauti na siku hizi, mtu akiajiriwa hana budi kumshukuru Mungu. Kazi hazipo nyingi, ziko chache kwa ajili ya watu wachache. Na ikizingatiwa kuwa Tanzania ina watu wengi sana na wasomi wamekuwa wengi, kupata ajira imeanza kuwa tabu kweli kweli. 

Tunawasihi vijana wafanye kazi kwa kujituma, na kwamba wasichezee kazi. Wazipende na kuziheshimu kazi zao, na wazifanye kwa uadilifu. Unapopata mshahara wako, ruksa kuuchezea kama unapanga kufanya hivyo, lakini siyo kuchelewa kazi. Kumbuka, wapo wengi ambao wangependa kupata nafasi yako, lakini hawana bahati hiyo. Kuwa mwangalfu kijana, utakuja kujuta na kwa bahati mbaya utakuwa umechelewa. Majuto ni mjukuu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Marafiki Ni Wengi Ukiwa Nacho

Next
Next

Fanya Maamuzi Kwa Mafanikio Yako