Marafiki Ni Wengi Ukiwa Nacho

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha, Mungu akikuwezesha ukawa na hali nzuri, jua kwamba utakuwa na marafiki wengi kila kona. Kati ya hao, wengine watakuwa ni wanafiki tu ambao wanataka wapate msaada kutoka kwako. Kwa kawaida, binadamu hupenda sifa. Ukiwa na marafiki wengi waliokuzunguka unaona raha na hivyo kutoa kwako haiwi shida kwa sababu unataka kujionyesha, unataka kila mtu atambue uwepo wako hapa duniani. 

Lakini cha ajabu, pamoja na kupenda kujionyesha kwa marafiki kuwa unacho na kuwa tayari kuwasaidia hao marafiki, ndugu zako wa damu ambao hawana kipato unawadharau na wala hauko tayari kuwasaidia hata kidogo. Utajifanya huwajui na wala huna habari nao kabisa. 

Lakini tukumbuke kwamba, duniani kuna kupanda na kushuka. Waswahili hunena, aliyekupa wewe ndiye aliyemnyima yule. Kibao hicho kinaweza kikageuka wakati wowote. Pale kitakapogeuka kibao na uchumi wako ukaporomoka, hali yako ikawa duni, utalazimisha kuwajua ndugu zako ambao kwa muda mrefu ulikuwa umewadharau. Wakati ukiwa hoi kiuchumi, marafiki wote watakukimbia na kwa vyovyote vile, hawatakuwa tayari kukusaidia. Badala yake wataanza kukucheka, kukudharau na kukudhihaki. Maneno kama, “tulijua tu staanguka…”

Yatupasa tuangalie sana. Katika maisha, kuna marafiki ndugu na marafiki wanafiki. Inabidi ujifunze kuwatambua ama sivyo utaishia pabaya. Tuwe makini katika kuchagua marafiki. Kamwe tusije tukawatupa ndugu zetu wa damu, kwani hao hata iweje, watakuwepo kwa ajili yetu. Tuwe makini.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Dunia Uwanja Wa Fujo, Kila Mwenye Ngoma Yake Hucheza

Next
Next

Usichezee Kazi, Chezea Mshahara