Dunia Uwanja Wa Fujo, Kila Mwenye Ngoma Yake Hucheza

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha ya wanadamu ni mapambano ya kila aina. Mapambano haya ni muhimu kwa ajili ya upatikanaji wa mahitaji muhimu kama vile chakula, mavazi na mambo mengine mengi. Kila anayeamka asubuhi anawaza la kufanya ili mradi siku ikamilike akiwa na chochote mikononi. 

Hebu jaribu kubana mahali asubuhi na kuangalia mikiki mikiki ya binadamu ilivyo. Utakuta kila mtu anahangaika na safari yake kiasi kwamba si rahisi kujua wapi anakwenda. Kuna anayeenda kulia na mwingine kushoto. Hakuna wa kumuuliza mwenzie wapi anakwenda, kila moja kivyake vyake tu. 

Kutokana na hali hii, ndipo unapogundua kuwa “dunia ni uwanja wa fujo” ambapo kila mtu ana mtindo wake wa kufanya hizo fujo. Baadhi ya fujo hizo zinaweza kuwa na mafanikio chanya na nyingine mafanikio hasi. Hali hii ama mikiki mikiki hii inatufanya tugundue kuwa dunia bila kupitia hayo tunayoita fujo haitasonga mbele. Kila mtu kwa fujo zake anazozifanya huleta mafanikio fulani ya sehemu husika. 

Duniani kote mambo yanafanyika hivyo, mitindo ya maisha iko hivyo ila tu inatupasa tufanye kazi kwa bidii na kwa njia sahihi. Yatupasa tufanye kazi kwa kutumia hekima ili mwisho wake uwe mzuri usiokuwa na fujo na matokeo yake yasikupeleke pabaya.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Siku Ya Kufanikiwa Ufurahi Na Siku Ya Mabaya Ufikiri

Next
Next

Marafiki Ni Wengi Ukiwa Nacho