Kamba Hukatikia Pabovu

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).

Kwa kawaida, mtu akiivuta kamba kwa nguvu, hakuna shaka, kama kuna sehemu mbovu kwenye kamba hiyo itakatikia pale pale palipo pabovu au palipolika na kuwa pembamba. Hii itatokea kwa sababu mahali hapo hapana nguvu, pana ubovu usioweza kuhimili kuvutwa huko.

Hali kadhalika, kwa mtu aliye mnyonge huwa ni hivyo hivyo. Mara zote mnyonge hulaumiwa kwa kufanya kosa fulani wakati ukweli siyo yeye, bali ni kuonewa tu kutokana na unyonge wake.

Usemi huu hutumika kuonyesha kwamba siku zote lawama huelekezwa kwa mtu aliye mnyonge. Watu wenye nguvu au wenye nafasi zao huwa hawalaumiwi na hata kama wana makosa, huwa hayaonekani. Ni sawa na kamba ambayo haina ubovu wowote, hata ingevutwa kwa nguvu kiasi gani, haiwezi kukatika.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Kikulacho Ki Nguoni Mwako

Next
Next

Bahati Humuendea Mwenye Kuitafuta