Ubora Ni Sumaku Ya Mafanikio

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ubora wa kitu huanzia kwenye mambo madogo madogo na katika ngazi ya chini kabisa ya kitu chenyewe. Ni dhahiri kuwa, kama huwezi kupika mchicha wa watu wawili vizuri ukavutia na ukawa na ladha nzuri, usitegemee kuwa siku ukiwa na mgahawa ndio utaweza kupika chakula kinachovutia. Pamoja na kwamba kila siku ujuzi huongezeka, na mtu kuweza kufanya vizuri zaidi, lakini kama tokea mwanzo ulikuwa hufanyi jambo lako katika ubora unaotakiwa, kwa hakika hata utakapopanda ngazi ya juu bado hutaweza kufanya kwa kuzingatia ubora.
Ni muhimu kuzingatia kuwa lolote unalolifanya kwa mikono yako, jitahidi kulifanya kwa umakini na kwa ubora zaidi kama vile hutalifanya tena. Kama wewe ni mhudumu wa ofisi, kama huwa unafagia, basi fagia kwa viwango na kwa ubora. Kama ni muuza mboga basi fanya kwa ubora wa hali ya juu ili uwe unasifika kwa kuuza mboga nzuri na zenye ubora. Hali kadhalika, kama wewe ni mama lishe, ambaye unapika na kuuza chakula basi pika, uza na fanya kwa ubora uliotukuka.
Tujifunze kuwa makini tunapoamua kulifanya jambo, ukiwa mtu wa kulipua lipua mambo, ina maana hata kama umeaminiwa kupewa kazi na mtu, haitakuwa rahisi kwako kufanya kilicho bora kwani huna tabia hiyo. Kila mara unapofanya jambo lolote kuwa na tabia ya kujifanyia tathimini hilo jambo ulilolifanya. Mafanikio yatakutafuta kama utaamua kufanya kwa ubora, hii ina maana kuwa kuanza jambo kwa ubora na kutenda kwa ubora. Tabia ya kulipua lipua haina mwisho mzuri, itakukosesha wateja na hata kipato.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania