Wanacheka Ukiwa Nao

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tuko katika ulimwengu wenye mambo mengi, vurugu nyingi na kila wakati tuko katika mapambano na kuneneana mabaya. Tatizo kubwa ni kutokupendana hasa pale tunapotofautiana kwenye uwezo wa kipato. Mara nyingi asiye na kitu ni mtu wa kutengwa na kutokusikilizwa katika jambo lolote. Mtu huyu huonekana kutokuwa na thamani yoyote na kwamba hawezi kuwa na mchango wowote wenye faida kwa jamii.
Binadamu tuna tabia ya kusahau na mara nyingi tunashindwa kujua na kutambua kuwa Mungu ana mpango na kila mja wake na kwamba mpango wa kila mtu unatofautiana na ule wa mwingine. Cha msingi ni kwamba kila mtu ana umuhimu wake mbele za Mungu. Kama vile ambavyo vidole havilingani, ukweli ni kwamba kila kidole kina kazi kwenye mwili wa mwanadamu.
Mara nyingi, binadamu huwa tunaangalia na kumthamini mtu mwenye nacho. Siku ambayo huyo mwenye nacho akipungukiwa kidogo basi ujue hakuna mtu atakayemsogelea kama ilivyokuwa zamani alipokuwa nacho. Hadhi ikija kushuka kidogo tu, basi hata wale ambao alikuwa akicheka nao watamcheka na kumsema vibaya.
Binadamu hatuaminiki, binadamu ndivyo tulivyo. Inapofikia hatua ya kuchekana na kusemana vibaya, ndipo utakapojua kuwa kumbe, mara nyingi, urafiki huwa hauna maana. Yatupasa kuwa makini na watu na marafiki tunaokuwa nao na kwa wakati gani. Binadamu hatuna wema, mara nyingi tunasahau maagizo ya Mungu aliyotuagiza, ya kuwa na upendo wa dhati na kweli baina yetu. Unafiki umekuwa sehemu ya maisha yetu, ni kipaumbele cha walio wengi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection