Mwenye Hekima Habishani

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ni rahisi sana kumjua mwanadamu ni wa aina gani ama kumjua jinsi alivyo. Hebu jaribu kumwambia mtu habari ambayo kwa hali ya kawaida inaweza kumkasirisha.
Subiri uone atakachofanya baada ya kusikia habari hiyo. Utamjua ni mtu wa aina gani kutokana na vile atakavyoipokea hiyo habari. Pengine mategemeo yako ama lengo lako lilikuwa ni kumuona amekasirika.
Unaweza ukashangaa jinsi atakavyoipokea habari hiyo. Utakachokiona pengine kinaweza kuwa ni tofauti na vile ulivyokuwa unafikiri. Kama mtu huyo ana busara hawezi kukujibu mara moja. Sana sana ataendelea kukusikiliza hata kama unamlazimisha aelewe vile unavyotaka. Wakati wewe unataka akuone umempa habari njema, yeye atakuwa anatafakari kwa makini hilo ulilomwambia.
Kwa kawaida, kimya hicho kinaonyesha kuwa huyu mtu ana hekima na hana tabia ya kukurupuka ama kuzungumza bila mpangilio. Kutokana na busara zake, anaweza akakujibu kuwa, “nimesikia”. Ni kawaida kwa wenye hekima kutumia muda wao kutafakari jambo kabla ya kulitendea kazi.
Kwa upande mwingine, kwa wale ambao hawana hekima, wao mara zote huwa ni wapayukaji na waropokaji wa maneno yasiyo na maana. Watu kama hawa huwa ni wachonganishi baina ya mtu na mtu ama baina ya watu na watu.
Mwenye hekima huwa ni mpatanishi na sio mchonganishi. Hekima huambatana na busara. Kwa bahati mbaya, karama hii inapatikana kwa watu wachache tu. Yatupasa sote tumuombe Mungu aweze kutupatia hekima katika maisha yetu ya kila siku.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection