Machozi Ni Nini?

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Machozi ni maji maji yanayotoka machoni, ila chimbuko lake ni moyoni kutokana na hisia kali, iliyosababishwa na tukio ambalo siyo la kawaida kwa mhusika. Kwa upande moja, linaweza kuwa tukio zuri sana sana kupita kawaida, au baya sana sana kupita kawaida. Aidha matukio mabaya au mazuri, yote yanasisimua hisia kali kwa mhusika, hisia ambazo zinaufanya moyo uitikie kwa kutoa machozi mithili ya bomba la maji yenye msukumo mkali.

Kwa hiyo msisimko mkali waweza kutoka nje ya mwili kwa njia ya machozi. Kulia kunapunguza ama kuondoa madhara yanayoweza kujitokeza kwa kuzibania ndani hisia hizo. Madhara hayo yanaweza kuwa kuzimia, shinikizo la damu, kiharusi au vidonda vya tumbo.

Machozi ni njia bora na salama inayoruhusu msukumo wa hisia kali ya mwili kumwagika nje ya mwili kwa usalama bila kumuathiri mhusika. Huzuni isiyotolewa nje kupitia machozi husababisha viungo vingine kulia, siyo kwa kutoa machozi bali kwa kupata maumivu ya sehemu mbalimbali za viungo kwenye miili yetu, hususani, kuumwa vichwa au hata kupata maumivu kwenye miguu.

Machozi ni dawa nzuri sana ya kuondoa ama kupunguza msongo wa mawazo. Kuna utaratibu fulani, sijui ni wa kimila ama wa kimfumo wa dume, ambao unawataka wanaume wasiwe wanalia. Utakuta mwanaume ana tatizo kubwa, mathalani, la kufiwa na mtu wa karibu sana, lakini kutokana na mwiko huo, mwanaume huyu atajikaza na kuumia ndani kwa ndani, atajizuia asilie. Mwiko wa wanaume hawa “kutoruhusiwa” kulia, hakujaacha wanaume wengi salama. Na pengine hii ni moja ya sababu kuwa na idadi ya wanaume wanaojiua kuwa juu zaidi ya ile ya wanawake.

Chonde, chonde kwa wanaume, toeni machozi kupunguza uzito ulilomo ndani ya mioyo yenu. Ninyi ni binadamu sawa na binadamu wengine, na
mna hisia kama wengine, hivyo, kulia ama kupiga kelele ni sahihi kabisa kwa kila mwenye pumzi hapa duniani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Maisha Ni Mlima Na Mabonde

Next
Next

Aisifuye Mvua, Imemnyea