Tenda Wema Nenda Zako

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha kwa ujumla ni mzunguko mkali sana. Mzunguko huo una mambo mengi mazuri na mengine mabaya. Tunaishi kwenye jamii kwa kusaidiana kwenye mambo mengi yanayotukabili. Binadamu siyo kisiwa hivyo kila mtu ana jukumu la kumsaidia mwenzie katika shida na raha. Tunavyofanya hivyo, tunategemea kwamba endapo jambo lolote litatokea kwetu pia, nasi tutasaidiwa vivyo hivyo.
Lakini, endapo itatokea wakati ukapata shida, na wale wote ambao walikuwa ni tegemeo lako usiwaone, utabaki unalalamika na kuwasema vibaya. Utakumbuka hata yale uliyowafanyia, lakini hiyo haitakuwa sahihi hata kidogo na haitapendeza. Yatupasa tufanye wema bila kutegemea kurudishiwa fadhila. Kumbuka, uliwatendea kwa wakati ule kutokana na kile ulichojaliwa kukifanya. Itabidi na wao wajaliwe pia ndipo waweze kukufanyia ama kuwafanyia wengine. Maisha ndivyo yanavyokwenda.
Inafaa ikumbukwe pia kuwa pengine hao uliowategemea wakusaidie, walikuwa hawana nafasi kwa wakati huo. Siyo lazima kila mtu asimame na wewe wakati unapowahitaji lakini watakuwepo wengine ambao watakuwa na wewe kwa wakati huo. Usihamishie tatizo lako kwa uliyemsaidia. Ni wachache wanajua kurudisha fadhila kwa waliyotendewa. Kati ya kumi waliosaidiwa, wanaweza kuwa wawili tu watakaorudi kutoa shukurani. Ndivyo mambo yalivyo, watu hawafanani.
Machungu ya jana usiyalete leo. Usiache kutenda wema kila iitwapo leo. Wapo watu ambao watakuwa tayari kukusaidia, watu ambao hujawahi kuwategemea hata siku moja. Dunia ndivyo inavyokwenda.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection