Usimwage Mtama Kwenye Kuku Wengi

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha ni mzunguko, tunakutana na mapito au matukio mengi ya kila aina kila uchwapo. Matukio yaweza kuwa mazuri, mabaya, ya aibu au ya kusikitisha. Kati ya hayo baadhi yanapaswa kuwa ya siri, na siyo ya kuanika hadharani kwenye kadamnasi. Endapo utayaanika hadharani, unaweza ukajikuta unajidhalilisha mwenyewe au unawadhalilisha wengine na mwisho wa siku ukasababisha mtafaruku mkubwa kwenye jamii.
Kutoa siri yako au ya mwingine kwa watu wengine haina maana ndiyo suluhisho la jambo hilo. Inapendeza sana pale unapokuwa na jambo linalokukereketa ukimweleza mhusika moja kwa moja ili aweze kujirekebisha pale inapobidi. Ukiwaeleza watu wengine ambao hawahusiki wanaweza kuwa wasambazaji wa habari hizo, na hiyo inakuwa siyo sahihi kabisa.
Hivyo tunashauriwa kuwa wasiri, washauri, na wapatanishi zaidi kuliko kuwa wasambazaji wa taarifa za watu au wasababishi wa mitafaruku katika jamii. Kuna mambo mengine hayapashwi kuongelewa kila Maharishi weweeee na kwa kila mtu na ndio kusudio haswa la usemi huu wa usimwage mtama kwenye kuku wengi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection