Baada Ya Dhiki Faraja

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Dhiki ni neno ambalo huwa sio zuri masikioni mwa walio wengi. Kwa ujumla, wengi huona kuwa ni neno lenye dhana ya udhalilishaji. Mtu anaposema, fulani ana dhiki, ina maana hajiwezi kwa mambo fulani fulani ambayo ni ya msingi na muhimu katika maisha yake.
Wakati mwingine, neno dhiki linaweza likatumika kama mtaji wa kukuwezesha kufikiri kufanya jambo fulani. Hakuna mtu anayeweza kufanya jambo bila kuwa na uhitaji. Mara nyingi, dhiki inakupeleka kwenye uhitaji. Katika hali hiyo utalazimika kutafuta uwezekano wa kutoka kwenye hiyo hali. Wakati huo ndipo dhiki inapobadilika kuwa mtaji.
Kwa sababu hiyo dhiki itakufanya kutafuta cha kufanya ili utoke kwenye hiyo hali. Hapo ndipo utakapofarijika kwani utakuwa umejitoa kwenye uhitaji huo. Katika maisha, watu wengi huanzia huko chini, yaani huanza wakiwa na maisha duni, ama maisha ya chini. Katika kupitia huko chini ndipo utakapoweza kukusanya shuhuda za kuwasimulia wengine kule ulikotoka. Utakuta mtu anawaambia wenzie, “Jamani, msinione hivi mwenzenu, nikiwasimulia niliyoyapitia huko nyuma, hamuwezi kuamini”.
Shuhuda za mafanikio huweza tia moyo wengine. Kama mtoa ushuhuda alipitia changamoto hizo, kwa nini na wengine wasijaribu ili waweze kufikia huko waliko mwenzao? Kila aliyefanikiwa, alianzia chini. Shuhuda zao zinakuwa na maana kwa jamii inayowazunguka. Kama ni watu wapendwa maendeleo, watajitahidi kufuata nyayo hizo ili nao waweze kufanikiwa.
Faraja haiji hivi hivi, ni lazima upitie magumu pamoja na dhiki lukuki. Tunaweza tukalinganisha usemi huu na ule wa “Mtaka cha Uvunguni Sharti Ainame”. Kuinama huko ni pamoja na mapito magumu utakayopambana nayo njiani ili uweze kufanikiwa.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection