Kila Jambo Na Wakati Wake

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha ya binadamu ni safari ndefu. Tunaweza kusema, maisha yana vipindi vikuu vinne, ambavyo ni:

  • Utoto
  • Ujana
  • Utu uzima
  • Uzee

Hatua zote hizi ni muhimu sana kwa mwanadamu na kila hatua ina taratibu za kuzingatia. Hebu tuchambue kipengele kimoja kimoja kama ifuatavyo:

UTOTO

Huu ni wakati wa raha kwani kila kitu unafanyiwa. Ni wakati wa kujifunza na kufuata maelekezo kutoka kwa wazazi na walezi. Lakini mtoto akishindwa kufuata mafundisho ya wazazi/walezi na wengine waliomtangulia, anaweza akaja akaharibiikiwa vibaya sana. Akiingia kipindi cha ujana anaweza kujikuta na matatizo mengi kutokana na kutofuata malezi hayo ya awali.

UJANA

Kipindi hiki kinaweza kuwa kigumu kwa vijana wengi. Ni kipindi ambacho vijana wengi hupenda kuiga iga mambo ya wana rika wenzao. Wanaweza wakaiga mabaya, hali kadhalika, wakiwa na bahati, wanaweza wakaiga mazuri. Kipindi hiki kinamuwezesha kijana uwezo wa kufanya kazi zinazomletea maendeleo. Vijana wengi, wasipoluwa waangalifu, hupotea kimaadili katika kipindi hiki. Vijana wanaaswa kuwa waangalifu sana katika kipindi hiki.

UTU UZIMA

Hiki ni kipindi ambacho mtu anakuwa na uwezo wa kufanya kazi akiwa na nguvu. Hata hivyo uwezo wake wa kufanya kazi siyo sawa na wakati alipokuwa kijana. Nguvu huanza kupungua kidogo kidogo. Huanza kuelekea kwenye uzee. Katika kipindi hiki, yatupasa kuwa waangalifu sana, hasa kwenye matumizi yetu, hususani ya pesa. 

UZEE

Ni kipindi ambacho mtu anakuwa hana nguvu imara za kufanya kazi zinazoweza kumletea maendeleo. Mara nyingi, huhitaji kutegemea vijana katika shughuli tofauti tofauti. Hiki huwa ni kipindi kigumu kwa wengi.

Usemi huu unatukumbusha na kutupa angalizo kupanga shughuli zetu kutokana na vipindi vyetu vya maisha tulivyonavyo. Hali kadhalika, hutupasa kuutumia muda wetu vizuri na kwa umakini, la sivyo tukizichezea ngazi hizo tajwa, hasa zile za ujana na utu uzima tunaweza kujikuta tunaharibikiwa mipango yetu yote ya kujiletea maendeleo yetu wenyewe na ya taifa zima kwa ujumla. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Moyo Ni Msitu

Next
Next

Baada Ya Dhiki Faraja