Bahati Humjia Kila Mtu Kwa Wakati Wake

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Binadamu tumeumbwa tofauti. Usemi huu unatufundisha kuwa kila binadam aliye hapa duniani, chini ya jua hili, ana siku yake muhimu ambayo ataikumbuka kwa uzuri.

Dhana iliyojengeka katika jamii ni kuwa aliyepata kapata. Kumbe kila mtu ana siku yake ambayo hakuna anayeijua zaidi ya yule muumba wetu. Lakini katika hilo, hiyo siku haiji kwa kukaa bure na kujibweteka. Inakuja kwa kujishugulisha kwa njia mbalimbali. Tatizo kubwa tulilo nalo sisi binadamu ni kukata tamaa pale tunapoona mambo hayaendi vile tunavyotaka.

Uzoefu unaonyesha kuwa pale unapoanza kukata tamaa, ndio ujue siku yako imekaribia kufika. Kama ulikuwa unapanda mlima ndio ujue unakaribia kufika kileleni. Waswahili husema kuwa mzigo huwa mzito wakati wa kuutua. Kamwe, usijifananishe na aliyetangulia, kwani naye alikuwa na safari yake. Tuache tabia ya kushindana, tusubirie siku yetu maana bahati humjia kila mtu. Haijalishi unapambana na mapito gani, lakini lazima bahati itakuja kwako pia wakati ukifikia.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ubaya Unavuma Kuliko Wema

Next
Next

Moyo Ni Msitu