Bandu Bandu Humaliza Gogo

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Siku zote jambo lolote linalofanyika huwa na mahali pa kuanzia. Mara nyingi mwanzo wa kila jambo huwa ni mgumu lakini ndivyo maisha yalivyo. Pengine, kwa wakati unapotaka kuanza jambo, inawezekana kulikuwa na ile hali ya kukata tamaa. Pengine unaona dhahiri kuwa jambo hilo haliwezekani kufanyika tena.
Tunaaswa, na hatutakiwi kukata tamaa. Kila jambo linaanzia chini, hakuna jambo linaloanzia juu. Kupambana ni wajibu, kupambana ni muhimu, kusotea jambo hadi lifanikiwe, pia ni muhimu. Kumbuka, ukipata kidogo ndio mwanzo wa kupata kikubwa zaidi. Mambo ni pole pole.
Kuna semi nyingi ambazo ni za maana sana katika maisha yetu. Usemi huu una maana ya kuwa kidogo kidogo ndio mwendo. Wengine pia husema mwenda pole hajikwai, na atafika aendako. Yatupasa kuwa na subira. Tujifunze kuwa kila jambo lina mahali pa kuanzia. Hata kwenye biashara unatakiwa kuanza chini, kidogo kidogo, mpaka kinaeleweka. Hata ule usemi wa Chovya Chovya, humaliza huyu la asali, una maana kubwa pia kwenye hali tunayoiongelea hapa. Kwa kudonyoa donyoa kidogo kidogo, hatimaye, utajikuta uko mahali pazuri. Hapo utakuwa na uwezo wa kushuhudia wengine. kile ulichokipata baada ya kupitia mlolongo wa mambo mengi.
Tatizo kubwa kwetu sote, hususani, vijana, ni kukata tamaa. Maisha hayaendi hivyo. Maisha ni mapambano na siyo maigizo. Pia usemi wa Mtaka cha Uvunguni, Sherti Ainame, una maana kubwa katika maisha yetu. Huwezi ukaokota kitu kilicho uvunguni ukiwa umesimama, kwa vyovyote, itakupasa uiname. Hayo ndiyo mapambano yenyewe tunayoyazungumzia.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection