Jungu Kuu Halikosi Ukoko

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika hali ya kawaida ya maisha ya kila siku, vyakula hupikwa kwenye vyombo mbalimbali. Vyombo hivi ni kama masufuria, vyungu na hata majungu makubwa, kulingana na shughuli iliyopo na mahitaji yake. Baada ya vyakula kuliwa kwenye shughuli yenyewe, huwa kuna mabaki au ukoko ambao kwa kawaida huwa hautupwi. Huwekwa ili endapo atatokea mtu mwenye uhitaji aweze kupewa. Wengi wameweza kupona kwa njia hii, waliweza kula wakashiba na hatimaye walishukuru kwa hicho walichopata.

Vilevile, katika maisha ya binadamu watu wazima na wazee, ingawa wamekula chumvi nyingi huwa wana mchango mkubwa sana katika maisha ya vijana kwani wanapoongea na vijana au watu wenye umri mdogo huongea maneno yenye busara na hekima ambayo huwaelimisha kimaisha na kuwapa mwongozo katika maisha yao. Wengi, vijana na hata watu wazima wameweza kuondoa msongo wa mawazo kwa kupitia busara za hao waliokula chumvi nyingi. 

Hivyo kutokana na umuhimu wa watu wazima na wazee, vijana mnapokuwa na changamoto mbalimbali katika maisha, mnapaswa kuwatafuta wazee au watu wazima waliowazidi umri ili muweze kupata nasaha na busara zao na hatimaye muweze kutatua changamoto zenu. Wahenga husema, “Jungu Kuu Halikosi Ukoko”, na wengine pia husema, “Uzee ni Dawa”, semi zote mbili zinaonyesha umuhimu wa kutambua na kuthamini uzee na busara zilizomo ndani ya vichwa hivyo vyenye nywele nyeupe.

Ukimfuata mzee kutaka ushauri / nasaha hutajuta, utafaidika hata zaidi ya ulivyotegemea. Hivyo, tunawasihi vijana msidharau au msione mnapoteza muda kwenda kupata ushauri au nasaha kutoka kwa wahenga kwani wana ukoko mwingi ambao unaweza kuliwa kwa faida katika maisha yenu.

Karibuni Ofisi ya TEWWY iliyopo Sinza  Makaburini ili muweze kupakuliwa busara pamoja na kupata nasaha ili hatimaye muweze kuondokana na msongo wa mawazo. Ushauri unatolewa bure.

Kwa maelezo zaidi, piga simu namba: +255 757 327 878

Karibuni sana!

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Changamoto Zako Zisikufanye Uwe Mbishi

Next
Next

Chimbuko La Urafiki Baina Ya Binadamu Na Mbwa