Usipoteze Muda Kutafuta Madhaifu Ya Watu

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ukimuona mtu anafanya vizuri katika eneo fulani, usimuandame. Hutakiwi kuanza kuyachunguza mambo yake mabaya, mapungufu yake pamoja na madhaifu yake kwa madhumuni ya kuyatangaza ili aonekane hafai mbele za watu. Badala yake, unatakiwa kumtia moyo na kumwombea. Endapo utashindwa kumuombea, basi umwache hivyo hivyo, alivyo.
Ukimuandama mtu huyo, Mungu wake aliyeamua kumng'arisha atakuja kukuaibisha wewe zaidi ya ulivyopanga kumuaibisha mwenzio. Usikubali kutumiwa na adui katika mashambulizi hayo, kwani mwisho wake siku zote huwa ni mbaya.
Ukiona Mungu ameamua kutembea naye pamoja na madhaifu yake madogo madogo aliyo nayo, ujue Mungu hajakosea na anajua anachofanya. Hutakiwi kabisa kuanza kutafuta habari zake mbaya za miaka 30 iliyopita ili tu umvunje moyo. Usifikiri kwa kufanya hivyo utashinda, la hasha. Kitakachotokea ni kinyume chake. Wewe ndiye utashindwa na utaharibikiwa sana. Hata siku moja, huwezi kuwa zaidi ya Mungu kwani Yeye ni kila kitu.
Najua unaweza ukawa na mengi ya kusema juu ya mtu fulani kwa sababu umeona amepata kibali mbele ya watu. Unaweza ukajua historia yake yote mbaya lakini ni vema usianze kuisema ili watu waache kumfuata, kumwamini au kumpenda. Tuwe watu wa kuona mema na kuyasema. Tujifunze kuficha aibu za wengine na hapo tutang'aa zaidi na zaidi mbele za Mungu na mbele za watu pia.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection