Kujiamini Na Bidii Katika Kazi Kunaleta Mafanikio Na Ushindi

Masimulizi
by Suzanne Njana (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mtu awaye yeyote anapofanya jambo lake kwa bidii hutarajia kupata mafanikio. Mafanikio huja kwa kujiamini na kuwa na bidii katika kufanya kazi. Mafanikio yenye ushindi hutokana na bidii na kujiamini katika kazi yako ili uyashinde madhaifu yanayoweza kujitokeza kufikia malengo yako.
Lakini kumekuwa na matatizo mengi yanayoonekana kwa watu wengi, hususan, vijana. Uvivu ndiyo tatizo kubwa sana kwa watu wengi. Uvivu unawafanya wasiwe wabunifu wa kutafuta mbinu mbalimbali za kupata mafanikio. Kutokana na kukosa ubunifu wamekuwa wakitekeleza mambo yao kwa wasiwasi au kimzahamzaha na mwisho wake kupata matokeo hasi ambayo huwa na athari kwa maisha yao. Kwa kawaida, mtu akikosa mafanikio, hukosa mwelekeo katika maisha na akikosa mwelekeo, mawazo huvurugika na hatimaye anafikia hatua ya kushindwa kuyamudu maisha yake.
Watu wengi, hasa vijana katika enzi hizi., wana mitazamo hasi. Ni jambo la kawaida kabisa kuwaona vijana wakiwa hawajitumi kufanya kazi ili wapate mahitaji ya kutosheleza maisha yao ya kila siku. Kazi ndio msingi wa maisha, bila kazi, maisha hukwama. Kukwama kwa maisha hupelekea mtu kukata tamaa, na wengine wakikata tamaa, moyo wa kujiamini hufa kabisa. Madhara yake, mtu kama huyu akipata shughuli ya kufanya ili iweze kumvusha, huwa hajiamini, utendaji wake hudorora. Kwa ujumla, anakuwa anazembea katika ufanyaji wa hiyo kazi na mwisho wa siku hushindwa kabisa.
Dhana ya kujiamini na bidii katika kazi inamhitaji kila mmoja awe nayo ili kuwa na mstakabali mzuri wa maisha. Kujiamini na bidii katika kazi ni misingi bora na imara katika maendeleo ya jamii na taifa kwa jumla. Maendeleo yakiwepo yatasaidia kupunguza idadi ya waliokata tamaa ambao inategemea kuwa wataiga mifano ya wenzao wenye bidii, waliofanikiwa. Kuwa na wivu wa maendeleo kunaruhusiwa. Kwa hiyo mtu akitaka kufanikiwa yampasa aangalie jinsi walivyofanya wengine na mbinu walizotumia hadi kufikia hatua hiyo. Ukijua mbinu unaweza kujaribu kuiga na pengine unaweza kufanikiwa. Kwa kufanya hivyo kutakuwa na jamii iliyo bora na iliyosheheni maendeleo.
Vijana wanaaswa wafanye shughuli zao kwa bidii, wajiamini na wajitume Ili waweze kutimiza malengo na waweze kupata mafanikio katika maisha yao. Mafanikio ya kijana mmoja, ni mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya taifa letu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection