Ganda La Muwa La Jana Chungu Kaona Kivuno

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Zoezi la kula muwa huanzia pale unapoumenya na kutupa maganda yake ambayo hayatafuniki. Sehemu ya muwa inayoliwa na binadamu ni ile nyeupe ya ndani baada ya kumenya. Sehemu hii nyeupe ndiyo tunayoitafuna na kupata majimaji matamu yenye sukari na kumeza. Mabaki yake baada ya kukamua utamu tunatupa.
Baada ya maganda na makapi meupe kukaa hadi kesho yake, huvunda na kutoa harufu nzuri ambayo humvutia Chungu. Chungu ni mdudu mdogo sana ambaye hupita kwenye mabaki hayo na kufyonza juisi ambayo kwake anaiona kuwa na thamani sana.
Methali hii ina maana na ina fundisho pia. Tunaona kuwa kile unachokidharau na kukiona kuwa kwako hakina thamani, kwa wengine huwa ni tofauti. Wewe unayekidharau unakitupa, mwingine mwenye uhitaji hukiokota kwani kwake anakiona kuwa ni cha thamani sana na ni mavuno au uhondo kwake.
Mfano mzuri unaoendana na methali hii ni ule wa mnunuzi wa nyama kutoka buchani. Mwingine akikuta nyama ya jana anaitaka hiyo hiyo wala haulizi maswali. Pengine, yule anayetaka nyama ya jana ana sababu zake. Anaona nyama ya jana imechuruzika maji na hivyo atapata nyama nyingi yenye uzito wa nyama yenyewe bila maji. Na pengine harufu ya nyama iliyolala inamvutia zaidi.
Mnunuzi mwingine anajisikia vizuri kununua nyama ya leo leo kwa sababu iko freshi na haina harufu. Mnunuzi huyu anaogopa kula vitu vilivyolala, pengine hapendi kuhatarisha afya yake. Huo ni uamuzi wake, unaheshimiwa pia.
Binadamu tuko tofauti. Kila mmoja ana maonjo tofauti na mwingine. Pale tunapotofautiana, inatupasa kuzikubali tofauti hizo kwani huo ndio uhalisia wa maisha ya mwanadamu. Binadamu hatuwezi tukafanana kila kitu, hiyo haitatokea hata siku moja.
Sisi Wanasihi wa TEWWY tunawapenda watu wote wenye uhitaji wa kupata ushauri kutokana na kuwa na matatizo ya afya ya akili. Tupo tayari kuwasaidia kwa kutoa unasihi. Lengo na madhumuni yetu ni kuwaona wakipona na wanakuwa na uwezo wa kuendelea na shughuli zao za kila siku. Haijalishi umesumbuka kwa muda gani. Tuko tayari kutumia kila njia kuweza kukuponya kwa kutoa unasihi wa mtu mmoja mmoja na hata katika vikundi. Pale tunapoona kuwa hali ya mteja inajitaji utaalamu zaidi, huwa tunampeleka mhusika kwenye ngazi za juu zaidi yetu.
Mwananchi, usiogope, usibaki na mizigo moyoni, ipo nafasi ya kuitulia mizigo hiyo, TEWWY ndipo mahali sahihi kwako. Utasaidika, haijalishi umekaa na tatizo kwa muda gani. Karibu!
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection