Mfinyanzi Hulia Gaeni

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mfinyanzi ni mtu anayejishughulisha na kufinyanga vyombo mbalimbali kama vile vyungu, vikaango, mitungi na vikombe. Kama ilivyo kwa wafanya biashara wote, mfinyanzi anafanya biashara akilenga kujiongezea kipato.

Kwa kuwa anafanya biashara, mambo ya nyumbani kwake anayaweka kando kiasi kwamba hata vyungu vilivyopasuka nyumbani kwake havipi kipaumbele kuvikarabati. Matokeo yake vyombo hivyo huendelea kutumika vikiwa vimepasuka ama kuvunjika pembeni hadi vinatia aibu mbele za watu.

Kutokana na hali hiyo, methali hii, "Mfinyanzi hulia gaeni" inaonekana kumgusa haswa mfinyanzi, kwani yuko tayari kulia chakula kwenye gae wakati uwezo wa kukarabati vyombo vyake ama kufinyanga vyombo vipya uko ndani yake. Na hii ni desturi ama tabia ya wafinyanzi wengi ya kutojali vyombo vya majumbani mwao. Kwa ujumla, hiyo tabia huwa haieleweki kabisa. Kusema ukweli, ni tabia ya kujinyanyasa ama tabia ya kutokujithamini.

Binadamu sote tunaaswa kuwa tusiendekeze sana pesa na kutokujali kwanza vitu vya nyumbani mwetu. Ni lazima tuthamini kwanza maisha yetu kwa kutumia hizo pesa tunazopata kutokana na kazi zetu ama kutokana na kazi za ufinyanzi. Hivyo, wafinyanzi mnaaswa kutumia vyombo bora majumbani mwenu. Acheni kutumia vyombo vilivyopasuka na kuharibika. Aidha mfinyange vingine ama mvifanyie ukarabati ili viwe katika hali ya unadhifu.

Kwa namna hiyo mtaweza hata kuvutia wateja wenu kwani wataweza kuona uzuri wa vyombo vyenu majumbani mwenu na hivyo kuona umuhimu wa wao pia kuwa navyo. Pale watakapoona vyombo mnavyotumia nyie wafinyanzi ni vibovu, hawataona sababu ya kuja kutengenezesha vyombo kwenye karakana zenu. Hivyo yawapasa mbadilike, acheni mambo ya kulia kwenye vigae.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Samaki Mkunje Angali Mbichi, Akikauka Hakunjiki

Next
Next

Kuna Wakati Wa Kuwaacha Au Kuwapoteza Uliowazoea