Mwamini Mungu Si Mtovu

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Alikuweko mtu mmoja na mkewe, hawakuwa na kitu, rasilimali yao kubwa ilikuwa ni kondoo na jogoo. Siku moja walipata habari kuwa rafiki yao alikuwa anakuja kuwatembelea. Mke alimwambia mume wake kuhusu ugeni huo. Alimkumhusha kwa kusema kuwa walikuwa hawana kitu chochote cha kumkirimu mgeni wao. Walichokuwa nacho ni huyo kondoo na jogoo. Lakini, mke aliongeza kuwa yeye asingependa kuwachinja wanyama wake, yaani kondoo jogoo.

Mume wake alimwambia, ikiwa hapatakuwa na budi labda watalazimika kumchinja kondoo. Wakati haya yanazungumzwa, kondoo na jogoo walikuwa wanasikia. 

Hata usiku moja, jogoo alianza kuwika kwa furaha. Maneno aliyokuwa akisema wakati akiwika ni haya: “Usiku uche tumchinje kondoo!” Na kondoo naye akawa anajibu, “Mungu ! Mungu”, maana yake, (mambo kwa Mungu). Jogoo akawika tangu saa tisa mpaka asubuhi kwa maneno hayo hayo: “Usiku na uche tumchinje kondoo!” Na kondoo hujibu , “Mungu! Mungu tu”

Hata kulipokuchwa hoja nyingine zikaanza. Mke akasema, bwana, huyu mgeni anayekuja ni mgeni wa siku moja, pana haja gani kumchinja kondoo kwa kitoweo cha siku tatu? Afadhali tumchinje jogoo. Basi alikamatwa jogoo akachinjwa. Kondoo ambaye alimtumainia Mungu alisalimika.      

Katika mazungumzo haya tunafundishwa kwamba tusikate tamaa tunapofanya shughuli zetu, hata pale tunapoona kuna dalili ya kushindwa. Yatupasa tuzidi kuongeza bidii na kumtegemea sana Mungu. Mara nyingi huwa tunakata tamaa tukisikiliza ya watu. Kwa kawaida, watu wengi hawapendi maendeleo ya wenzao. Huwa hawapendi kuona wenzao wanafanikiwa katika maisha. Wanaweza wakakuletea visababu mbalimbali vya kukukatisha tamaa. Lengo lao wanataka ushindwe, usione hatima yako. 

Hatutakiwi kukubalina na fikra zao potofu. Lazima tujitambue na tujithamini kwa kila tunachofanya. Tujitahidi kuachana na marafiki ambao wanaweza wakatupoteza tukashimdwa kutimiza malengo yetu. 

Kuna msemo unasema “ Bora adui kuliko rafiki anayejua kila kitu unachokifanya.” Rafiki wa aina hiyo anaweza akakupoteza vibaya sana. Epukana na marafiki wa namna hiyo. Kaa mbali nao.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Kawia Ufike

Next
Next

Kaa Mbali Na Mazoea