Kawia Ufike

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kukawia ni kuchelewa au kutofika kwa wakati unaotakiwa. Wanaposema kawia ufike wana maana chelewa lakini ufike mahali unapotakiwa kuwa. Msemo huu unatumiwa sana na baadhi ya watu wasiojitambua na wasiokuwa na uhakika wanatakiwa wafanye nini. Sehemu za ibada ni moja za sehemu ambazo watu hutumia sana msemo huu. Wanapoutumia msemo huu kwenye masuala ya nyumba za ibada, wanakuwa na maana kuwa hata wakikawia, ili mradi watakuwa wamefika, haijalishi sana. Kwa wanaosema hivi ina maana kuwa, cha muhimu kwao ni kuonekana kuwa walikuwepo ili mradi wasieleweke vibaya.
Lakini watu hao hao wakiitwa kwenye mahojiano ya kutafuta kazi, wanawahi hata saa nzima kabla ya muda uliotakiwa. Hapa inaonyesha, ni kitu gani katika maisha wanakitilia maana zaidi. Kile ambacho wanaona ni cha maana zaidi, basi watakipa uzito hicho na kuwahi kama inavyotakiwa.
Mimi binafs, sikubaliani na usemi huu. Ningependa, kama ni kazini au sehemu ya ibada tuwahi ili tuweze kupata kinachotakiwa. Unapokawia kufika, inaonekana kama jambo hilo ama shughuli hiyo huitilii maanani ama unafanya kwa ulegevu kwa makusudi mazima. Kiukweli, tabia hii si nzuri katika maisha.
Vijana wanaaswa kuwa msemo huu hauwafai. Yawapasa waamue kufika mapema ili waweze kupata mambo yote yanayohitajika kutoka kwenye shughuli yenyewe. Mambo ya kuzembea zembea yatawakosesha mengi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection