Kilio Cha Mbuzi Hakimzuii Kupelekwa Sokoni

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Hapa duniani, kuna matukio mengi sana ambayo yanatukuta kila siku za maisha yetu sisi wanadamu. Matukio mengine huumiza na mengine yanafurahisha. Dunia ndivyo ilivyo. Endapo matukio yote yangekuwa yanafanana, kwa hakika yangeweza kutuchosha, wengine husema, yange-boa.

Matukio yaumizayo ni kama yale ya kuondokewa na mpendwa wako, kama vile mzazi, mtoto au mume/mke. Hawa watu ni miongoni mwa watu ambao ulikuwa unawapenda sana, na hata pengine walikuwa ndio tegemeo lako kubwa. Kuondoka kwao huwa ni pigo kubwa sana.

Matukio yafurahishayo ni kama vile kupata mtoto, kufaulu kwenye masomo, kufunga ndoa na mengine mengi tu, Orodha ni ndefu. Kwa vile yanafurahisha, furahia kwa kiwango/kiasi utakachoweza, ni haki yako.

Ukipata matukio ama mambo ya kuhuzunisha kama yaliyotajwa hapo juu, ya kuondokewa, nayo tunatakiwa tuyapokee kwani ni sehemu ya maisha. Hatutakiwi kukesha na kulia huku tukilaumu kwa nini yamekukuta wewe n.k. Utafanya yote hayo, utalalama wee, lakini haitasaidia chochote. 

Unachotakiwa kufanya ni kunyanyuka na kusimama imara na kuyakabili kwa ujasiri. Maisha ni lazima yaendelee, hivyo endelea kufanya shughuli zako kama kawaida. Hayo yaliyokutokea ni ya kawaida na ni lazima yatokee kwa kila mtu. Ndivyo Muumba wetu alivyopanga, hakuna wa kushindana naye hapo. Sote, safari zetu za hapa duniani ni fupi sana na hivyo hatuna budi kuyapokea machungu hayo kwenye maisha yetu. 

Tunaaswa tunapopatwa na masahibu hayo, tusikae chini, kulia na kuomboleza bila kikomo, kamwe hakutasaidia. Maisha ni lazima yasonge mbele, upende, usipende, ndivyo ilivyopangwa. Hakuna njia mbadala. 

Daima yatupasa tukumbuke kuwa, vilio vyetu haviwezi kamwe kubadilisha taratibu za Muumba wetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Mchumia Juani Hulia Kivulini

Next
Next

Kawia Ufike