Tutumie Mikakati Thabithi Katika Kuwafunza Watoto Wetu Maadili Mema

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Hapo zamani kulikuwa na kaka mmoja ambaye alikuwa akiwalea dada zake wawili. Aliwapenda sana na akawa karibu nao. Aliwalea vizuri na kuwapatia mahitaji yao ya msingi. Kuhakikisha usalama wa dada zake, alijenga ukuta mrefu kuzunguka nyumba waliyokuwa wakiishi. Pia alihakikisha kuwa  milango ya nyumba ilikuwa imara kabisa. Kila siku jioni alifunga milango yote yeye mwenyewe. Baada ya kufunga milango, aliita majina ya dada zake wote ili kuhakikisha kuwa wapo chumbani kwao. Dada zake wakiitikia, anajiridhisha kuwa mambo ni shwari. 

Kujitaabisha kote huko ilikuwa ni kulinda heshima ya familia yao. Aliogopa kupata fedheha ya dada zake kupata mimba kabla ya kuolewa. Hakutaka kabisa aibu ya namna hiyo itokee.

Jitihada zake za ulinzi wa dada zake hazikuzaa matunda. Cha kushangaza, mmoja wa dada zake alipata kile alichokuwa hakitarajii kitokee. Alipata uja uzito. 

Kwa taharuki, kaka alichukua bunduki. Alitaka huyo dadake mjamzito amweleze imekuwaje mpaka ikawa hivyo. Dada yake naye bila kusita, alimjibu kaka yake  akasema, “kaka hili karavati kubwa kama la barabarani ulilojenga, lilingia hadi uani kwetu ili kutoa maji machafu. Kila siku jioni tulikua tunasafisha na maji safi na hapo ndipo mahali nilikua natokea kwenda kukutana na mvulana wangu. Nilikuwa narudi asubuhi sana kabla nyie hamjaamka". 

Kaka alibaki mdomo wazi, ameduwaa asijue la kusema, wala la kufanya. Alifikiria jitihada zake alizozifanya za kuwalinda dada zake. Aliumizwa sana na hili tukio la dadake kupata mimba. Kwa hakika kufanya mambo bila mipango thabiti huwa hakuzai matunda. Kuzungushia ukuta mrefu kama wa magereza na kutengeneza milango imara hakukuwa suluhisho kwa kile alichokuwa akitaka kaka kisitokee kwa dada zake.

Tunajifunza nini kutoka simulizi hii? 

Tunajifunza umuhimu wa wazazi na walezi katika kuwalea watoto vizuri na kwa mikakati. Tukumbuke kuwa tunaishi na binadamu ambao kila moja ana akili zake. Kuzungushia ukuta peke yake bila kuwapa elimu ya kutosha ya namna ya kujitunza, haisaidii. Watoto wanapaswa kuambiwa bayana madhara yanayoweza kutokea wakijiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo. Muda zaidi utumike na wazazi/walezi katika kuwapa elimu kuliko kuzungushia ukuta mrefu ili kuwazuia watoto wasitoke nje ya geti. Watoto wanaweza kubuni njia mbalimbali za kujinasua kwenye vifungo wanavyopewa na wazazi/walezi wao. Watoto wanapaswa kufundishwa namna ya kuthamini utu wao na kwamba kila kitu kina wakati wake.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Acha Kuishi Kwa Wasiwasi, Hapo Ulipo Bado Una Nafasi

Next
Next

Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo