Tuwe Tayari Kufanya Kazi Wakati Wote

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kujitolea ni kufanya kazi bila kulipwa. Watu wengi hawajitolei kutokana na ukweli kwamba huwa hakuna malipo. Watu hupenda kulipwa hata kama kuna neno kujitolea limewekwa. Binadamu ndivyo tulivyo.

Kulikuwa na Muuguzi mmoja wa hospitali na mama mmoja mjamzito ambao walisafiri ndani ya basi moja kwenda Bukoba. Wasafiri hawa wawili walikuwa hawajuani. Wakiwa bado safarini, uchungu wa kuzaa ulimuanza yule mama. 

Mungu bariki, Muuguzi alikuwa amejizatiti vizuri, alikuwa na vitendea kazi vinavyohitajika kwa kazi iliyo mbele yake. Alikuwa na moyo mkuu wa kujitolea. 

Muuguzi alisogea karibu na yule mama mjamzito baada ya kuona dalili za uchungu zikiwa zinamnyemelea kwa kasi. Alichukua hatua za kumpima na akagundua kuwa yule mama alikuwa amefikia hatua ya kujifungua. 

Alimwomba dereva asimamishe basi kituo kinachofuata ili wampeleke mama yule Zahanati.

Basi lilisimama, kisha

wakampeleka Zahanati iliyo karibu. Pale Zahanati, wauguzi walishirikiana hadi mama alipojifungua. Mama alijifungua salama mtoto wa kike.

Mama aliyejifungua alipumzika kwa muda kidogo. Baadaye walirudi kwenye basi kwa furaha na mtoto wao. Abiria pia walifurahi kuwa sehemu ya kushuhudia tukio hilo muhimu. Hali kadhalika, abiria walimpongeza Muuguzi kwa kuutendea haki ujuzi wake. Abiria walimpa mtoto zawadi nyingi na wakampa jina la basi husika. Na hatimaye waliendelea na safari hadi wakafika mwisho wa safari.

Tunajifunza nini kutoka tukio hili?

Tunajifunza umuhimu wa kuwa tayari na kujituma wakati wowote, na katika mazingira yoyote. Kila mtu ana jukumu la kujitoa kwa moyo kushirikiana na kusaidiana na jamii. 

Kisa hiki kinashabihiana na usemi wa, "Tenda Wema Nenda Zako Usingoje Shukurani." Ikumbukwe kuwa huyu muuguzi alikuwa hamfahamu yule mama mjamzito. Lakini kutokana na utu na ubinadamu wake, muuguzi aliweza kujitoa na kumsaidia huyo mama katika hali aliyokuwa nayo, bila kujali kama anamjua ama laa. Utayari wa kutoa msaada inapohitajika ni muhimu kwa kila mmoja wetu hapa duniani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Maji Ya Moto Hayaunguzi Nyumba

Next
Next

Nyoka Na Jongoo