Nyoka Na Jongoo

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Hapo zamani za kale, Nyoka alikuwa ana miguu lakini macho hakuwa nayo. Jongoo naye alikuwa na macho, lakini miguu alikuwa hana. 

Wawili hao walikubaliana kuwa marafiki. Waliahidiana na kukubaliana kuwa, kila mmoja baina yao, akitaka kitu kwa mwenzie, itampasa apate. 

Hata siku moja Nyoka akamwambia Jongoo, rafiki yangu, leo kuna ngoma huko Rufiji. Naomba uniazime macho yako nikatazame ngoma. Jongoo naye akapewa miguu ya Nyoka. 

Baada ya hapo, Nyoka akatoka akaenda kutazama ngoma. Na Jongoo akawa amekaa pale pale kwani hakuweza kwenda popote maana alikuwa haoni. 

Ngoma ilipokwisha, Nyoka alianza kurudi nyumbani. Lakini alipofika nusu ya safari, akatazama huko na huko, akaona faraja kubwa kuona vitu vizuri. Akawaza moyoni mwake na kujisemea, “wajua Jongoo anafaidi, anaona vitu vizuri, tena anaweza kuwaona hata adui wakiwa mbali. Basi ya nini nimrudishie? Yeye na aitwae miguu yangu na mimi nitayatwaa haya macho yake”. 

Baada ya kufanya maamuzi hayo kimoyo moyo, aliamua kugeuza njia akaenda upande mwingine. Mzee Jongoo akabakiwa na miguu mingi bila macho. 

Nyoka alikaa na macho yake. Tangu wakati huo Nyoka na Jongoo hawakupatana tena.    

Yako mengi ya kujifunza kwenye simulizi hii. Somo kubwa sana tunalopata ni  

kwamba yatupasa tuache tamaa, turidhike na tulichonacho. Mara nyingi tunaangamia kwa sababu ya kujifananisha na vile wanavyoishi wengine. Mara nyingi kujilinganisha huku ama kuwa na tamaa ya kuwa kama ‘yule’, kunatupeleka pabaya. Hatimaye, tunaishia kupata roho ya tamaa ya kwa nini nisifanye hivi ili nipate zaidi niweze kufikia maisha kama ya fulani. 

Ulicho nacho kidogo, ambacho Mungu amekupa ni kikubwa kuliko kile utakachopata kwa njia ya dhuluma. Tujifunze kuridhika na maisha yetu huku tukifanya kazi kwa bidii ili kuweza kuboresha maisha yetu. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Tuwe Tayari Kufanya Kazi Wakati Wote

Next
Next

Ukomo Wa Subira Yako Ndio Mwanzo Wa Husuda