Ukomo Wa Subira Yako Ndio Mwanzo Wa Husuda

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kila jambo linalofanywa na mtu yeyote lina mahali pa kuanzia. Katika kuanza jambo kunahitajika mipango thabiti ili liweze kutekelezeka. Utekelezaji wa mipango hiyo, utahusisha binadamu wengine kwa asilimia kubwa. Kwa kawaida, kipindi hicho huwa ni cha mpito. 

Hakuna kitu kilicho kigumu kama kusubiri mtu akuwezeshe kutatua matatizo yako. Mara nyingi, ahadi zinakuwa ni nyingi na wewe ukiwa na mategemeo kuwa mambo yote yatakuwa sawa. Sasa ikitokea kuwa umeshindwa, lawama zinaanza kuja mfululizo. Huyu atasema vile, na mwingine atasema hivi, ili mradi tu kila mtu atakuona kuwa hutaki kutoa msaada. 

Katika kipindi hicho ndio husuda huanza. Husuda ni chuki kutoka kwa mhitaji akijua kuna mtu wa kumsaidia. Akiwa katika mategemeo hayo, atajitahidi kuwa karibu sana na wewe. Atatafuta maneno mazuri ya kukupamba na kukusifia bila ukomo. Lakini pale itakaposhindikana kupata msaada, hapo ndipo husuda, chuki na lawama vitaanza dhidi yako. Mazuri yote aliyowahi kufanyiwa yatasahaulika kabisa. 

Ukishindwa kutoa, utaonekana kuwa na roho mbaya. Hawatajua kuwa hauko kwenye nafasi ya kusaidia kwa wakati huo. Husuda pia husababisha hata watu kuumizana. 

Pengine usemi wa “Mtumai cha ndugu hufa masikini” ni sahihi mahali hapa. Watu wengi hupenda kutegemea zaidi msaada kutoka kwa ndugu na marafiki zaidi kuliko wao wenyewe kujitengenezea mipango yao ya kuwavusha kutoka kwenye umaskini.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Nyoka Na Jongoo

Next
Next

Wazazi Wana Haki Ya Kutunzwa Na Watoto Wao