KUWA MAKINI, CHUNGUZA USHAURI UNAOPEWA KABLA YA MAAMUZl

Simulizi
by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ushauri ni maoni yanayotolewa kwa mtu ili yamsaidie kupata suluhisho kwenye changamoto anazopitia. Aidha, ushauri ni maelekezo ya kitaalamu yanayotolewa kwa mtu yeyote ili kumwezesha kufanya jambo fulani.
Binadamu anategemea akili zake katika kupanga mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake ili aweze kutimiza ndoto zake. Kuna wakati mambo yanakuwa magumu kuyatolea maamuzi, hivyo hupaswa kuwashirikisha wengine kwa ushauri zaidi kwani wanaweza wakawa wa msaada kutokana na uzoefu walio nao.
Watu wanaoweza kutoa msaada ni pamoja na watalaam, ndugu, jamaa na marafiki. Wakati mwingine mtu anaweza kukwama kufikia malengo yake endapo atapewa ushauri mbaya usiokuwa na mafanikio. Kwa mfano, mwanafunzi wa Sekondari asipopata ushauri mzuri kwenye uchaguzi wa masomo ya mchepuo anaweza akapoteza mwelekeo wa fani si taaluma inayomfaa.
Hali kadhalika wafanyabishara wasipopata ushauri mzuri kibiashara wanaweza kukosa mwelekeo wa biashara zao. Ushauri unahitajika katika kila ngazi ya maisha. Binadamu tunategemeana kwa kila hali, maisha ndivyo yalivyo.
Nini tunajifunza kutoka maelezo ya hapo juu?Hapa tunasisitizwa kuwa makini kuangalia na kuchuja ushauri unaofaa na ambao haufai kwa maendeleo ya maisha yetu. Hatutakiwi kuchukua kila kitu kutoka kwa washauri wetu. Yatupasa tuufanyie kazi ushauri mzuri tunaopewa na watu wenye uzoefu. Ushauri mbaya tuuache pale pale usije ukatuharibia malengo yetu ya maisha.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection