"Malezi Ruksa" Yana Athari Kwa Watoto

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Malezi Ruksa (Permissive Parenting) ni aina mojawapo ya malezi ambayo mtoto anapewa ruksa ya kufanya au kuchagua chochote anachopenda/anachotaka bila ya kudhibitiwa. Malezi haya humpa mtoto uhuru uliopitiliza kiasi kwamba mtoto anasahau wajibu wake. Hata hivyo, hii ni aina ya malezi inayomfanya mzazi ajione anampenda sana mtoto wake.
Ni kweli kwamba mtoto anastahili malezi bora ikiwa ni pamoja na kupewa mahitaji muhimu ambayo ni chakula, malazi, afya, elimu na haki nyingine za msingi. Mahitaji yasiyo ya lazima kwa mfano; pipi, baiskeli, kagari kadogo, toi ya silaha, baluni, chokoleti simu, au pesa ni ya kuacha.
Kutokana na malezi ruksa, mtoto hajui kama kuna neno hapana kwake, yeye kila jambo ni ndiyo tu kila siku. Hivyo hajui kama kuna kukosa chochote kile anachohitaji, anajua ni lazima apate tena kwa wakati. Laiti mtoto angaliomba kitu akaambiwa hakipo, hakuna pesa au nitakununulia nikipata pesa, angeona ni jambo la kawaida, hatimaye angeizoea hiyo hali.
Malezi ruksa yana athari nyingi kwa mtoto ambazo ni pamoja na; kupoteza mwelekeo wa maisha kwani anashindwa kukabiliana na changamoto anazokutana nazo. Mtoto anashindwa kujitegemea. Malezi hayo yanazalisha wazazi (mke na mume), wote waliodekezwa tangu utotoni. Wazazi tujiulize, Je kizazi kitakachozaliwa chenye kudekezwa, kitakuwaje?
Wazazi tunatakiwa tufanye nini?
- Tuhakikishe tunawapatia watoto wetu mahitaji muhimu na tuzingatie haki zao.
- Tuwalee watoto katika njia ipasayo ikijumuisha: kiakili, kiafya, kimwili, kitabia, kihisia, kiroho, kimazingira na hata kijamii.
- Tusiwapende watoto kupitiliza kwani tunawadekeza na kuwaharibia maisha yao ya baadaye.
- Wazazi tuwe makini kuleta kizazi bora na si bora kizazi. Tukifanya hivyo, yaani kuwa na bora kizazi, tutakuwa kwenye madeni makubwa hapa duniani na huko mbele ya safari.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection